IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /65

Amri kuhusu Talaka katika Sura At-Talaq

16:44 - March 07, 2023
Habari ID: 3476670
TEHRAN (IQNA) - Uislamu umelipa kipaumbele maalum suala la familia na kuzingatia majukumu na wajibu maalum kwa kila mwanafamilia ili waweze kuishi pamoja kwa upendo na amani.

Uislamu pia una suluhisho kwa wale wanandoa ambao wana migogoro mikali na hawawezi tena kuishi pamoja. Hili limezungumziwa katika Sura At-Talaq.

At-Talaq ni sura ya 65 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 12 na iko katika Juzuu ya 28. Ni Madani na Sura ya 99 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Talaq kwa Kiarabu maana yake ni talaka. Zaidi ya nusu ya Sura inahusu kanuni zinazohusiana na kutengana kwa mume na mke kwa msingi wa mafundisho ya Uislamu, na ndio sababu sura ikapewa jina hilo.

Katika sehemu ya kwanza ya Sura, kanuni za jumla kuhusu talaka zimetajwa pamoja na onyo, vitisho na habari njema.

Pia inazungumzia haki za wanawake waliopewa talaka na wale walio wajawazito wakati wa talaka. Kisha Sura inataja hatima ya mataifa na jamii zilizotangulia kama somo.

Sehemu ya pili ya sura inaangazia ukuu wa Mwenyezi Mungu, malipo kwa watu wema na adhabu kwa watenda maovu.

Inahusu hatima ya makundi mawili: Wale waliomuasi Mwenyezi Mungu na watapata adhabu kali na wale waliomtii Mwenyezi Mungu na kutenda kulingana na mafundisho ya Manabii watukufu wakapokea mwongozo maalum wa Mwenyezi  Mungu na watafurahia baraka za peponi.

Pia inazungumzia masuala kama vile Tauhidi, Siku ya Kiyana na Utume, inasisitiza haja ya Taqwa (kumcha Mungu) na mwanadamu kumtegemea Mwenyezi Mungu.

3482721

captcha