IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 58

Sura Al-Mujadila: Maana ya Hizbullah kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu

16:23 - January 21, 2023
Habari ID: 3476439
TEHRAN (IQNA) – Qur’ani Tukufu inawataka waumini wa kweli kujiunga na Hizbullah. Leo, Hezbullah imekuwa neno lenye maana ya kisiasa. Kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu Hizbullah ni neno lenye maana ya kidini na kiitikadi na neno hili kimsingi maana yake ya moja kwa moja ni 'Chama cha Mwenyezi Mungu'.

Jina la sura ya 58 ya Qur'ani Tukufu ni Al-Mujadila. Ina Aya 22 na iko katika Juzuu ya 28 ya Qur'ani Tukufu. Ni Madani na ni Sura ya 106 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Neno Mujadila maana yake ni yule anayejadiliana na jina la Sura linatokana na malalamiko ya mwanamke dhidi ya mwenzi wake.

Sifa makhsusi ya Surah Al-Mujadilah ni kwamba ni sura pekee ya Qur'ani ambamo ndani yake neno Mwenyezi Mungu limetajwa katika aya zote. Maudhui ya Sura yanaweza kugawanywa katika sehemu tatu:

Sehemu ya kwanza ni kuhusu sheria za talaka kabla ya Uislamu na kisha inaelezea maoni ya Uislamu juu yake.

Sehemu ya pili inazungumzia adabu za maingiliano na wengine na jinsi ya kuzungumza na Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Na katika sehemu ya mwisho, tabia ya mnafiki inajadiliwa. Ni wale ambao kwa dhahiri wanafuata Uislamu na kupendelea malengo yake lakini wana mafungamano ya siri na maadui wa Uislamu.

Sura inawaonya Waislamu kutowafuata wanafiki, kundi linaloelezewa kuwa ni “Chama cha Shetani”.

Pia inawashauri Waislamu wa kweli kuwa marafiki na wale ambao wako kwenye njia ya Mwenyezi Mungu na wawe maadui na wale ambao hawako  katika njia na kisha inawaalika kujiunga na ‘Hizbullah’.

Hizbullah katika Sura hii hairejelei kundi ambalo limewekewa mipaka kwa jamii, lugha au eneo fulani, bali inahusu waumini wa kweli ambao hawafanyi urafiki na maadui wa Mwenyezi Mungu na ambao matendo yao yako kwenye njia ya Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo kila muumini thabiti, haijalishi anaishi wapi duniani na anazungumza lugha gani, ni mwanachama wa Hizbullah.

captcha