IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /61

Taswira ya Wanafunzi wa Nabi Isa katika Sura As-Saf

22:19 - February 12, 2023
Habari ID: 3476549
TEHRAN (IQNA) – Katika kila zama katika historia ya wanadamu, waumini wamejitahidi kulinda dini na kukabiliana na ukafiri. Hili ndilo lililofanywa na wanafunzi waaminifu wa Nabii Isa au Yesu –Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe JuuYake- wanaojulikana kama Hawariyun.

Quran Tukufu inazungumza juu yao katika Sura As-Saf.

As-Saf ni sura ya 61 ya Qur’ani Tukufu ambayo ina aya 14 na iko katika Juzuu ya 28. Ni Madani na ni Sura ya 111 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Neno Saf, ambalo maana yake ni wale waliosimama katika safu, linakuja katika Aya ya nne ya Sura na linarejea kwenye safu ya wale wanaofanya Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana."

Kumtukuza Mwenyezi Mungu, na kuwaonya wale ambao vitendo vyao vinatofautiana na maneno yao, ushindi wa mwisho wa dini ya Mwenyezi Mungu na kuenea kwake duniani kote na ubatili wa majaribio ya wapinzani  ya kuzuia dinia ya Mwenyezi Mungu kuenea duniani kote. Aidha sura inawahimiza kushiriki katika Jihadi kwa mali zao na maisha yao.

Aya ya nane inayowalingania Waislamu kushiriki katika Jihadi kwa   njia ya Mwenyezi Mungu na kukabiliana na maadui wa dini. Inasema: “Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.”

Sura pia inasema Mtume wa Uislamu, Muhammad (SAW) ameteuliwa kwenye nafasi hii na Mwenyezi Mungu ili aweze kuwaalika watu kwenye dini ya kweli, dini ambayo habari njema yake ilikuwa imetolewa kwa Bani Isra’il na Nabii  Isa (AS).

Imesisitizwa katika Sura As-Saf kwamba waumini hawapaswi kuwahimiza wengine kufanya yale ambayo wao, wao wenyewe, hawafanyi na kwamba lazima watimize ahadi zao. “Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda?” (Aya ya Pili)

Katika aya ya mwisho, Hawariyun wanaelezwa kuwa ni masahaba au wanafunzi maalumu wa Nabii Isa(AS): “Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!...’”

Moja ya aya zinazojulikana za Sura ni Aya ya 13: “Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” Baadhi ya wafasiri wanasema habari ya ushindi ni juu ya kutekwa kwa Makka wakati wa Mtukufu Mtume (SAW) wakati wengine wanaamini inahusu ushindi wa mwisho wa waumini katika mwisho wa zama.

captcha