IQNA

Hija katika Uislamu/3

Ibada ya Hajj, safari yenye thamani

21:17 - October 29, 2023
Habari ID: 3477805
TEHRAN (IQNA) – Hija ni safari yenye thamani sana kiasi kwamba wale wanaosafiri kwa ngamia hawapaswi kupanda ngamia anayekula uchafu.

Hija si safari rahisi na ya kawaida. Ni dhihirisho la Uislamu.

Uislamu una miundo mitatu: Ni Qur’ni Tukufu katika umbo la maneno, ni muundo wa binadamu (mkamilifu) katika sura ya Maimamu maasumu watoharifu, na ni kitendo au amali katika umbo la Hajj.

Kila wakati tunapotafakari safari hii ya kiroho tunapata mambo mapya kuihusu.

Ka’aba Tukufu ni bendera ambayo chini yake tunapaswa kukusanyika na kupaza sauti ya Tauhidi (Imani ya Mungu mmoja). Hapo tunakumbuka historia na Siku ya Kiyama.

Kuangalia mandhari ya Makka kunatufasiria Qur’ani Tukufu. Qur’ani Tukufu inasema: “Haki imedhihiri na uwongo umetoweka”? Wako wapi watu kama Abu Jahl waliotaka kumuua Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kuzuia ujumbe wake usienee?

Katika Hija kuna utaratibu wa kushangaza. Mahujaji hufanya ibada katika maeneo fulani, kwa wakati fulani katika mwelekeo fulani na kwa madhumuni fulani.

Hija hufanywa kwa kuzingatia kalenda ya mwezi ya Hijri na, kwa hivyo, wakati mwingine huja wakati wa msimu wa baridi na wakati mwingine katika msimu wa joto. Mahujaji hawapaswi kuogopa baridi wakati wa baridi na joto katika majira ya joto.

Hijja ni dhihirisho la Aya ya 50 ya Surah Al-Adhariyat: "Jikinge kwa Mwenyezi Mungu."

Tunaposwali, tunajitenga na vitu vya kimaada kwa muda mchache, vivyo hivyoo katika saumu ambayo hudumu kwa masaa machache na halikadhalika katika Hajj kwa siku chache.

Hija ni dhihirisho la Aya ya 99 ya Surah Saffat: “Nitakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Ataniongoza.”

Kuelekea katika njia ya Mwenyezi Mungu na kutekeleza ibada za Hija ni lazima kuwe chini ya usimamizi wa mwanachuoni na kwa kuzingatia Fatwa (maamrisho) ya mwanazuoni aliyefika daraja ya juu zaidi katika elimu ya Kiislamu yaani Marjaa Taqlid. Hivyo kabla ya kuanza safari ya Hajj, tunapaswa kuhakikisha Salah yetu inatekelezwa kwa usahihi. Tunapaswa kuamua Marjaa na pia tutekeleza maamurisho ya Uislamu kuhusu malipo ya kifedha kama vile Zakat na Khums ili tusiwe na tatizo katika safari hii ya kiroho.

Kujitolea, kuzingatia kanuni za maadili, kusaidia wengine, kusali na kutafakari mengi, na kuzingatia sana adabu za hija ni muhimu katika safari hii ya kiroho.

Kishikizo: ibada ya hija
captcha