IQNA

Wanawake katika Uislamu

Naibu Mkuu wa UN asisitiza mchango wa wanawake katika Ustaarabu wa Kiislamu

22:15 - November 08, 2023
Habari ID: 3477861
JEDDAH (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amesema wanawake wametoa mchango wa ajabu katika ustaarabu wa Kiislamu.

Hata hivyo, alisema, katika nchi nyingi bado wanaachwa nyuma. Akihutubia mkutano wa kimataifa mjini Jeddah kuhusu haki na nafasi ya wanawake katika Uislamu, alitoa wito wa kuchukuliwa hatua katika nyanja za elimu, uwezeshaji wa kiuchumi na amani.

Mkutano huo ulifanyika mjini Jeddah, Saudi Arabia, siku ya Jumatatu. Bi. Mohammed alisema ameheshimiwa kuwa sehemu ya mjadala wa "jinsi gani tunaweza kurudi kwenye maono ya awali na mazuri ya Uislamu ya kumpima mtu si kwa jinsia yake bali kwa nguvu ya imani zao na wema wa matendo yao."

Alikumbuka kwamba tangu mwanzo, Uislamu ulitambua haki ya wanawake kushiriki katika kufanya maamuzi ya kisiasa, kurithi, na kumiliki mali na biashara, “lakini karne nyingi baadaye, katika nchi nyingi na katika nyanja nyingi za maisha, wanawake wameachwa nyuma.”

Bi. Mohammed alitoa wito wa kutenda kwa mshikamano katika nyanja tatu "kurekebisha makosa." Alisema mengi zaidi lazima yafanywe ili kupata haki ya elimu kwa watu wote, hasa wanawake na wasichana, "kwa sababu Qur'ani Tukufu inatutaka tufanye hivyo".

Pia alizungumzia maafa ya kibinadamu yanayotokea Gaza, akisisitiza kulaani kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa mauaji ya raia, na wito wake wa kusitishwa kwa mapigano na ufikiaji usiozuiliwa kwa watu wanaohitaji.

"Sisi, katika eneo hili na dunia, lazima sote tufanye kila tuwezalo kumaliza ukatili huu wa kutisha, maumivu, na mateso na kurejea kwenye meza ya amani, labda tu wakati huu na wanawake," alisema. "Imani yetu ya Kiislamu inatudai kwamba tuwajali majirani zetu wakati wa shida."

3485922

Kishikizo: wanawake waislamu
captcha