IQNA

Wanawake 21 wanaharakati wa Qur'ani Kuenziwa

18:33 - May 11, 2016
Habari ID: 3470305
Kongamano la Saba la Kuwaenzi Wanawake Wanaharakati wa Qur'ani litafanyika sambamba na Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Masoumeh Farzaneh, mshauri wa Shirika la Awqaf la Iran amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa wanaharakati 21 wa Qur'ani kutoka Iran na nchi kadhaa wataenziwa katika kikao hicho.

Ameongeza kuwa wanawake 450, wakiwemo 150 kutoka nchi 80, waliwasilisah kazi zao katika kongamano hilo kuhusu harakati zao Qur'ani.

Farzaneh ameongeza kuwa, makongamano yaliyopita yalisaidia kuleta maingiliano mazuri baina ya wanawake wanaharakati wa Qur'ani nchini Iran na maeneo mengine ya Waislamu duniani.

Awamu ya 33 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran inaanza Jumatano hii kwa muda wa wiki moja chini ya kauli mbiu ya "Kitabu Kimoja, Ummah Moja".

3496791

Kishikizo: wanawake waislamu
captcha