IQNA

Mtazamo wa Maadili Katika Qur'ani/ 3

Qur'ani Tukufu inasemaje kuhusu kushuku au dhana mbaya

19:00 - March 06, 2024
Habari ID: 3478462
IQNA-Aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi zinatuhimiza tuepuke shubuha, kushuku na kutoaminiana. Kuwashuku au kuwa na dhana mbaya kuhusu wengine ni tabia mbaya ambayo inaweza kuwa na athari hasi kwa mtu na wale wanaohusishwa naye.

Kuwa na dhana mbaya na kuwashuku wengine ni tabia mbaya ambayo inaweza kuwa na athari mbaya kwa mtu na wale wanaohusishwa naye.

Kwa mujibu wa Uislamu, kushuku au kuwa na dhana mbaya ni dhambi. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 12 ya Surah Al-Hujurat:

“Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa?…”

Qur'ani Tukufu inasema jiepushe na dhana nyingi kwa sababu tuhuma nyingi dhidi ya watu.

Ikiwa mtu huwa na mashaka na wengine mara nyingi, itamfanya kuwa na tabia mbaya kwa wengine, na watapoteza kumwamini.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 12 ya Suratul-Fath: “Lakini mlidhani kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana mbaya, na mkawa watu wanao angamia.”

Hii ina maana kwamba tuhuma huharibu moyo na tabia ya mtu.

Katika aya nyingine, Qur'ani Tukufu pia inatahadharisha dhidi ya kumshuku Mwenyezi Mungu:

 Na awape adhabu wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanao mdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. . (Aya ya 6 ya Suratul-Fath)

Dhana mbaya waliyokuwa nayo juu ya Mwenyezi Mungu ni kwamba walidhani ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake hazitatimia na Waislamu hawatawashinda maadui. Hata hivyo, walipata ushindi dhidi ya maadui na ahadi ya Mungu ilitimia.

Kwamba wanafiki na makafiri wana shaka juu ya Mwenyezi Mungu lakini waumini hawana shaka kama hiyo ni kwa sababu wanafiki na makafiri wanaona Dhahiri ya matukio lakini waumini wanazingatia ukweli na kiini cha mambo.

Vyovyote iwavyo, Qur'ani Tukufu inapinga vikali tuhuma na dhana mbaya inaonya juu ya adhabu kali juu yake.

3487386

captcha