IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /23

Jinsi ya kupata baraka zaidi za Mwenyezi Mungu

22:58 - August 28, 2023
Habari ID: 3477512
TEHRAN (IQNA) – Ni swali la kawaida kwa watu kuuliza jinsi gani wanaweza kupata baraka nyingi za Mwenyezi Mungu.

Jibu la swali hili ni kushukuru kutokana na neema ulizopata. Kumshukuru Mungu kwa baraka ambazo ametupa kuna matokeo mengi chanya katika maisha ya watu na ni hali yao ya kiroho na kiakili.

Qur’ani Tukufu inasisitiza umuhimu wa kushukuru na athari zake katika maisha.

Kulingana na Aya ya 7 ya Sura Ibrahim, kuwa mwenye shukrani huongoza kwenye baraka zaidi: “Na alipo tangaza Mola wenu Mlezi: Mkishukuru nitakuzidishieni; na mkikufuru, basi adhabu yangu ni kali.”

Kwa hivyo kushukuru kuna athari nyingi chanya katika nyanja tofauti za maisha, pamoja na zifuatazo:

1- Uhusiano wa mwanadamu na Mwenyezi Mungu

Mtu anayemshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake kwa hakika anasema anastahili baraka zaidi na Mwenyezi Mungu anamwongezea baraka anazopokea. Ndio maana Imam Ali (AS) anasema ni kwa shukrani kwamba baraka zinaendelea.

2- Uhusiano wa mtu na wengine

Kama vile kumekuwa na msisitizo wa kuwa na shukrani kwa Mwenyezi Mungu, kuwa na shukrani kwa watu kwa ajili msaada pia ni jambo ambalo limesisitizwa. Ikiwa mtu anajiona kuwa ni wajibu kwa wengine, husababisha maelewano zaidi na huruma katika jamii na jamii kama hiyo inaweza kuhimili kila tukio na tishio.

Kwa mujibu wa Hadith kutoka kwa Imamu Ridha (AS), mtu ambaye hana shukurani kwa watu wengine hana shukurani kwa Mungu, Mwenyezi pia.

Qur’ani Tukufu  pia inasema kuwa kushukuru kuna faida kwa mtu mwenyewe: " Na tulimpa Luqman hikima, tukamwambia: Mshukuru Mwenyezi Mungu. Na mwenye kushukuru basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na aliye kufuru, basi Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Msifiwa.” (Aya ya 12 ya Surah Luqman)

Sifa mbili za Ghani na Hamid (Mwenye kujitosheleza na Mwenye kusifiwa) katika Aya hii ni msisitizo wa ukweli kwamba Mwenyezi Mungu hahitaji shukurani zetu bali ni vyema kwetu kupokea zaidi baraka zake.

captcha