IQNA

Maadili katika Qur'ani /2

Ubabe na ukaidi humpelekea mtu kupotea

18:16 - June 07, 2023
Habari ID: 3477115
Kwa kawaida watu hawapendi kuwa chini ya udhibiti wa wengine au imani yoyote. Wanapenda kuishi kwa uhuru lakini wengine hawajui nguvu ya ndani inayowaweka mbali na uhuru wa kweli.

Ubabe wa kiitikadi na ukaidi ni mambo mawili yanayomshika mtu na kumpoteza.

Ubabe wa kiitikadi na ukaidi ulikuwa miongoni mwa sababu zilizofanya watu washindwe kukubali wito wa manabii wa Mungu.

Ubabe wa kiitikadi unamaanisha kushikamana kupita kiasi kwa jambo fulani, kama vile imani, kiasi kwamba mtu hutoa muhanga ukweli kwa ajili hulka hiyo. Ukaidi nao unamaanisha kusisitiza juu ya jambo fulani na kukataa kubadilisha maoni ya mtu ingawa ni kinyume na akili na mantiki. Wenye ukaidi wakati mwingi huwa wamashabaini ukweli uko wapo lakini kutokana na kiburi chao hukataa kukubali ukweli.

Watu waliokataa kuwafuata Mitume wa Mwenyezi Mungu wameelezwa katika Qur'ani Tukufu ifuatavyo:  "Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!" (Aya ya 7 ya Surat Nuh)

Kulingana na aya hii, ushabiki wao ulikuwa mwingi kiasi kwamba walikataa hata kusikiliza ukweli achilia mbali kuukubali.

Sababu na mantiki ni mambo ambayo yanatoa mwelekeo kwa hatua za mtu. Wale wasiotii mantiki na akili na kujaribu kwenda kinyume na njia ya asili hawatashindwa tu bali pia kupoteza kila kitu walicho nacho. Ubaguzi na ukaidi ni mambo yasiyo na maana yanayompelekea mtu kupotea.

Hakuna sababu au mantiki inayoathiri tabia na mwenendo wa mtu ambaye ana ubaguzi. Anaangalia matukio jinsi anavyopenda sio jinsi yalivyo. Wanasisitiza njia yao mbaya na wanakataa kusikiliza sababu yoyote.

Qur’ani Tukufu katika aya mbalimbali inawataja watu wa aina hiyo ambao wamenaswa na ushupavu na ukaidi.

  • Wanaofuata njia ya wazee wao bila ya kuuliza akili zao. “Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.” (Aya ya 23 ya Surah Zukhruf).
  • Ubaguzi ni miongoni mwa sababu za ubaguzi wa rangi: “Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini." (Aya 198-199 za Surat Ash-Shu’ara)
captcha