IQNA

Utamaduni

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu atembelea Maonyesho ya Vitabu ya Tehran

14:11 - May 13, 2024
Habari ID: 3478812
IQNA: Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran na kuweza kufahamu kwa karibu kuhusu sekta ya uchapishaji nchini.

Kwa mujibu wa idara ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Vitabu leo ​​(Jumatatu) ambayo yanafanyika katika Eneo la Sala la Imam Khomeini (RA). Akiwa katika maonesho, Kiongozi Muadhamu alizungumza na wachapishaji, waandishi na wamiliki wa maduka ya vitabu, na kufahamishwa kwa karibu kuhusu habari za uchapishaji na hali ya soko la vitabu, pamoja na kiwango cha kukubalika kwa maonyesho hayo. Maonyesho hayo yalizinduliwa Jumatano iliyopita, yakikaribisha zaidi ya wachapishaji 2,500 wa Iran na 60 wa kigeni ambao wamewasilisha vitabu vyao vipya zaidi katika hafla hiyo. Yakiendeshwa chini ya kauli mbiu "Tusome na Tuunde," Maonyesho ya 35 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yataendelea hadi Mei 18. Yemen imepewa hadhi ya mgeni maalum katika maonyesho hayo ya vitabu mwaka huu kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa muqawama au mapambano ya Kiislamu. 4215459

 

captcha