IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Tunisia: nakala 6,000 za Qur’ani zasambazwa

19:15 - May 03, 2025
Habari ID: 3480631
IQNA – Zaidi ya nakala 6,000 za Qur’ani Tukufu zimegawiwa kwa wageni katika Maonyesho ya 39 ya Vitabu ya Kimataifa ya Tunisia.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah na Uongofu ya Saudi Arabia imetolea nakala hizo. Usambazaji  ulianza wakati maonyesho yalipoanza tarehe 25 Aprili, kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la Saudi. Maonyesho yataendelea hadi tarehe 4 Mei.

Katika banda la Saudia, wageni wanaweza kuona mkusanyiko mkubwa kutoka kwa Taasisi ya Mfalme Fahd Complex ya Uchapaaji wa Qur’ani Tukufu, ikiwa ni pamoja na tafsiri za maana za Qur’ani Tukufu na Misahafu ya aina mbali mbali. 

Wageni wa banda hilo pia wanaweza kunufaika na programu za kielektroniki zinazoshirikisha maudhui ya elimu na huduma za kidini.Miongoni mwa vivutio ni programu ya 3D ya Hajj na Umrah, ziara za kina za Msikiti Mkuu wa Makkah na Msikiti wa Mtume huko Madina kwa mbinu ya 'Virtual Reality'.

Inafaa kuashirikia hapa kuwa, Virtual Reality ni teknolojia inayounda mazingira yanayoshabihiana na yake kweli na hivyo kumfamnya mtazamaji wa taswira kudhani yuko katika eneo husika analolitazama.

3492913

Habari zinazohusiana
captcha