IQNA

Nidhamu Katika Qur'ani / 14

Qur’ani Tukufu inasemaje kuhusu utaratibu na nidhamu katika shughuli za kiuchumi

22:55 - May 15, 2024
Habari ID: 3478829
IQNA – Qur’ani Tukufu inasisitiza kwamba mali ya jamii haipaswi kukabidhiwa kwa watu ambao hawajakua au kukomaa katika masuala kifedha au kiuchumi.

Moja ya vigezo vya ustawi wa kifedha na kiuchumi ni mipango na nidhamu katika sera, tabia na mwenendo.

Mali kwa mtu binafsi imefananishwa na uti wa mgongo wa mtu. Ndiyo maana watu ambao ni maskini hawawezi kusimama kwa miguu yao wenyewe kifedha.

Qur’ani Tukufu inasisitiza kwamba mali haipaswi kukabidhiwa kwa mjinga. “Msiwape watu wanyonge mali zenu ambazo Mwenyezi Mungu amekufanyeni kuzisimamia. (Aya ya 5 ya Surah An-Nisa)

Ikiwa mpumbavu atapewa uti wa mgongo wa jamii, atauvunja na hivyo kuiangusha jamii.

Sifa mojawapo ya mtu asiye na uelewa ni kutojua kutumia na kufaidika na mali. Kwa mtazamo wa Qur'an, ili mtu awe na mamlaka ya mtaji na mali, anahitaji sio tu ukomavu bali pia ufahamu wa masuala ya kifedha. Qur’ani Tukufu inasema kuhusu mayatima:

 Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.” (Aya ya 6 ya Surah An-Nisa)

Kwa hivyo kulingana na aya hii, mayatima wanapaswa kupimwa juu ya ujuzi na ufahamu wao wa masuala ya kifedha na wasaidiwe katika ustawi wa kifedha.

Mipango na nidhamu katika tabia ni miongoni mwa vipengele muhimu vya usimamizi wa masuala ya kifedha na uchumi.

Mojawapo ya misingi ya nidhamu ya kifedha  ni kuepuka kuahirisha mambo. Mtukufu Mtume (SAW) alisema ole wao wanaoakhirisha mambo ya watu kuanzia leo hadi kesho!

Amirul Muuminin, Imam Ali (AS), alimshauri Malik Ashtar kufanya baadhi ya mambo yeye mwenyewe, kama vile kuwajibu watu na kutimiza matakwa yao siku hiyo hiyo.

Imam Ali (AS) pia anasisitiza kwamba mtu anapaswa kufanya kila kitu kwa wakati sahihi na kuepuka kuchelewesha.

3488234

Kishikizo: Qurani Tukufu.
captcha