IQNA

Nidhamu Katika Qur’ani /12

Umuhimu wa Unadhifu Kwa mujibu wa Uislamu

23:13 - May 12, 2024
Habari ID: 3478810
IQNA – Katika Uislamu, hasa katika Sira ya Mtukufu Mtume (SAW), kuna msisitizo mkubwa juu ya unadhifu na usafi dhahiri wa sura.

Moja ya maana ya nidhamu ni kuwa nadhifu. Moja ya ishara za watu ambao hulipatia umuhimu suala la nidhamu ni kwamba wao huwa pia na unadhifu. Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amesema Mwenyezi Mungu ni mzuri na anapenda uzuri na anapenda kuona athari za baraka zake kwa waja wake.

Pia imepokewa kutoka kwa Mtume (SAW) kwamba Mwenyezi Mungu hampendi mtu mchafu na mwenye kunuka.

Qur’an Tukufu, katika Aya ya 32 ya Surah Al-Aaraf, inaashiria umuhimu wa kutumia mapambo:

Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.

Kwa mujibu wa aya hii, makafiri pia wanaweza kunufaika na mapambo ya hapa duniani lakini katika Siku ya Kiyama, yatakuwa ni ya Waumini tu.

Katika Aya ya 31 ya Sura hii, Mwenyezi Mungu anawaamuru watu “Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu. 

Kwa hivyo imependekezwa watu wawe na mapambo na wawe nadhifu katika jamii, katika maingiliano na wengine, na hasa misikitini na wakati wa Sala kwa sababu wakati wa Swalah, mtu anaswali kwa aliye mwenye uzuri zaidi (Mungu).

Unadhifu katika misikiti pia huhimiza wengine wawe nadhifu na hujenga hali ya utulivu na kuvutia. Bila shaka, mapambo yasiwe kwa kiasi kwamba yanawafanya maskini au wasiojiwezi kuhisi vibaya na pia yasiwe ni chanzo cha kuwadhuru wengine.

Nukta nyingine ni kwamba mapambo katika aya hizi yanaweza kumaanisha mambo ya kimwili na ya kiroho kama vile nia safi na tabia njema.

3488209

Kishikizo: Qurani Tukufu.
captcha