Hafla hiyo imeandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wa Utawala wa Kiroho wa Waislamu wa Kyrgyzstan, Shirika la Habari la Saudi (SPA) liliripoti Jumanne.
Mashindano ya mwaka huu yalianza katika majimbo saba na miji miwili, yakishirikisha washiriki 270 katika awamu za awali.
Washiriki wanashindana katika kategoria nne: kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 20, kuhifadhi Juzuu 10, na usomaji wa Qur’ani Tukufu na Tajweed.
Duru ya mwisho iilianza siku ya Jumanne kwenye Msikiti wa Imam Sarakhsi huko Bishkek.
Wageni wakuu katika sherehe za kufunga siku ya Jumatano watajumuisha Abdulaziz Zakirov, Mufti na mkuu wa Utawala wa Kiroho wa Waislamu wa Kyrgyzstan; Dk. Awad Al-Enezi, Naibu Waziri wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu Saudia, Balozi wa Saudi nchini Kyrgyzstan Ibrahim Al-Radi; wabunge kadhaa; na vyombo mbalimbali vya habari rasmi.
Shindano la kwanza, lililofanyika Desemba 2023, liliandaliwa katika ngazi ya kitaifa kwa wavulana. Saudi Arabia inasema mashindano hayo ni sehemu ya mipango ya kimataifa ya wizara hiyo yenye lengo la kuendeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu na Sunnah na kukabiliana na misimamo mikali.