IQNA

Msichana mwenye ulemavu wa macho Misri ahifadhi Qur'ani kwa muda wa miezi 18

12:32 - December 30, 2021
Habari ID: 3474744
TEHRAN (IQNA)- Roa'a al Sayyed, msichana mwenye umri wa miaka 11 aliye naulemavuu wa macho nchini Misri amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu kwa muda wa miezi 18.

Roa'a yuko katika darasa la sita na anaishi katika moja ya vijiji vya jimbo la Dakahlia. Amekuwa akihudhuria chuo cha kuhifadhi Qur'ani katika kijiji chake. Mkuu wa chuo alichohudhuria Ehab Al Shariff anasema Roa'a ni mwanafunzi mwenye nidhamu na ameshinda zawadi kadhaa katika mashindano ya kieneo ya Qur'ani. Aidha amesema binti hiyo ana mustakabali mweme kutokana na unyenyekevu na kipawa chake.

Mmoja wa waalimu wake, Salim Baker anasema Roa'a ni chanzo cha furaha kwa chuo hicho na amesema binti huyo huwapa matumaini wanafunzi wenzake.

Amedokeza kuwa Roa'a ameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kutumia ipasavyo simu yake ya mkononi yenye aplikesheni ya kuhifadhi Qur'ani.

Aidha amesema masomo yake ya Qur'ani yamemsaidia kufanya vyema zaidi katika masomo mengine ya shule.

Sherehe za kumueni Roa'a imefanyika katika chuo hicho na kuhudhuriwa na maafisa wa serikali katika eneo hilo.

3477120

captcha