IQNA

Binti Msyria mwenye ulemavu wa macho afunza wenzake Qur'ani katika kambi ya wakimbizi

19:41 - January 29, 2021
Habari ID: 3473602
TEHRAN (IQNA) – Zuhra Darzi Alwash ni binti kutoka Syria anayeishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya nchi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.

Yeye ni msichana mwenye umri wa miaka 15 na ana ulemavu wa macho lakini hilo halijawa kikwazo katika maisha yake kwani hivi sasa anawafunza watoto Qur'ani Tukufu katika kambi hiyo ya wakimbizi.

Zuhra na familia yake waliukimbia mji wao wa jadi wa Idlib mwaka 2019 baada ya kuvamiwa na magaidi wakufurishaji. Baada ya safari ya muda mrefu waliwasili katika kambi walimo hivi sasa. Zuhra alizaliwa akiwa na ulemavu wa macho na hivyo hana uwezo wa kuona lakini ana kipaji maalumu cha kuhifadhi aya za Qur'ani.

Binti huyu hakubahatika kuenda kuenda shule na hivyo hajui kusoma wala kuandika lakini aliweza kujifadhi Qur'ani kwa kusikiliza kanda za wasomji maarufu.

Zuhra anasema anatamani sana siku moja aweza kuanza masomo ya shule ili ajue kusoma na kuandika. Kwa sasa anatumia muda wake wote kuwafunza watoto Qur'ani Tukufu.

3950236/

captcha