IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanawake wenye ulemavu wa macho

16:18 - November 08, 2021
Habari ID: 3474528
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur'ani maalumu kwa wanawake wenye ulemavu wa macho yameandaliwa hivi karibuni nchini Iraq.

Kwa mujibu ya waarifa mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani yalifanyika kwa njia ya intaneti katika Idara ya Masomo ya Qur'ani ya Chuo Kikuu cha Umm al Banin ambacho kinafungamana na Mfawidhi wa Haram Takatifuya Hadhrat Abbas AS.

Ali al Bayati, mkuu wa idara hiyo amesema mashindano hayo ni kati ya harakati za Qur'ani ambazo huandaliwa ili kuwaunga mkono wanawake wenye ulemavu wa macho.

Mashindano hayo yalisiammiwa na jopo la majaji ambao wote pia walikuwa maeneo mbali mbali ya Iraq.

Mshindi wa mashindano hayo alikuwa ni Ruqaya Adib wa Baghdad akifuatiwa na Aya Imad wa Diyala huku nafasi ya tatu ikishikwa na Ayat Zia wa Baghdad.

Visually-Impaired Women Attend Online Quran Contest

4011483

captcha