Israil iliripoti kucheleweshwa tukio hilo, shirika la habari la Quds limeripoti
Kikao hicho kilipangwa kufanywa huko Casablanca kwa ushiriki wa wasomi wa Kiyahudi na. Kiislamu.
Spika wa bunge la Morocco pia alipangwa kulihutubia kikao hicho.
Waandalizi wameahirisha tukio hilo kwa hofu kwamba watu waliokasirishwa na vita vya mauaji ya halaiki vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza watafanya maandamano makubwa.
Mkutano huo umeakhirishwa mara mbili hapo awali, mara moja mwezi Mei,2024 na mara nyingine mwezi Juni, 2024.
Bado hakuna tarehe mpya iliyotangazwa ya mkutano huo.
Wananchi wa Morocco wamekuwa wakifanay maandamano makubwa makubwa tangu Desemba 10, 2020 kupinga hatua ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala wa kifalme nchini humo na utawala wa Kizayuni wa Israel katika makubaliano yaliyosimamiwa na utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Raia wa Morocco Wahimiza Kususia Biashara Zinazounga mkono utawala huo wa Israeli, Wataka Kukomeshwa kwa Kuhalalisha.
Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuhalalisha utawala mwaka huo. Nyingine zilikuwa Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan.