Jumuiya ya Ahul Bayt: Ujerumani imekiuka sharia katika kufunga Kituo cha Kiislamu Hamburg
IQNA - Shirika moja lisilo la kiserikali la kimataifa lenye makao yake makuu nchini Iran limelaani vikali marufuku ya Ujerumani dhidi ya Kituo cha Kiislamu cha Hamburg (IZH) na kuitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa wazi wa mikataba ya kimataifa, pamoja na haki za binadamu na uhuru wa dini, kujieleza na kukusanyika.
Katika taarifa yake siku ya Ijumaa, Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl Al-Bayt (AS) imezitaka mamlaka za Ujerumani kufuta marufuku ya kutatanisha kwa kituo hicho.
Kauli hiyo ilitolewa siku moja baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani kusema kuwa imepiga marufuku Kituo cha Kiislamu cha Hamburg, inayojulikana zaidi kwa Msikiti wake wa Bluu au Msikiti wa Imam Ali, na mashirika yake tanzu kote Ujerumani kwa kuendeleza kile ilichokiita "itikadi kali za Kiislamu na za kiimla."
Wizara hiyo ilisema majengo 53 ya IZH yalikuwa yamepekuliwa katika majimbo manane ya Ujerumani, kwa kufuata agizo la mahakama.
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl Al-Bayt (AS) ilisema "inalaani vikali hatua inayokinzana na uhuru wa dini na haki za kimsingi za binadamu."
Ilielezea IZH kama moja ya vituo muhimu zaidi vya kidini, kisayansi na kitamaduni nchini Ujerumani, ambayo kwa zaidi ya miaka 60 imekuwa ikitenda "ustadi" katika nyanja za mafundisho ya kidini na ya Kiislamu, na pia kukuza mazungumzo na kuishi pamoja kwa amani huku ikikataa msimamo mkali, mifarakano, na vurugu.
"Kuleta mashtaka dhidi ya kituo hicho, ambacho kimekuwa kikwazo dhidi ya itikadi kali, ukufurishaji na migogoro, hakuna msingi kabisa kutoka kwa mtazamo wa kisheria na wa kibinadamu," ilibainisha jumuiya hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani ikiwa ni pamoja na kuhujumiwa vituo vya Kiislamu.
3489260