Msikiti Mkuu wa Kufa, ulioko takriban kilomita 12 kaskazini mwa Najaf, Iraq, ni moja ya misikiti muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia, unachukuliwa kuwa msikiti wa nne kwa umuhimu baada ya Masjid al-Haram jijini Makka, Al-Masjid an-Nabawi jijini Madina na Masjid al-Aqsa jijini Al Quds.
Msikiti huo unaoaminika kuwa ulijengwa na Mtume Adam (AS), una historia ndefu na umekuwa ukitembelewa na Mitume na mawalii mbalimbali wakiwemo Mtume Muhammad (SAW), Imam Ali (AS), Imam Hassan (AS) na. Imam Hussein (AS).
Pia una makaburi ya watu mashuhuri kama Muslim ibn Aqeel, Hani ibn Urwa, na Al-Mukhtar, na umezungukwa na maeneo ya kihistoria, pamoja na nyumba ya Imam Ali (AS).
3489629