Msikiti wa Kufa pia ni kati ya athari za kale na muhimu katika mji huo. Aidha katika msikiti huo kuna Mihrabu ya Imam Ali (AS) ambayo ni sehemu alipokuwa Imamu huyo mtukufu wakati alipopigwa dharba kwa upanga na ibn Muljam al-Muradi katika usiku wa 19 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka wa 40 Hijria Qamaria.