Hussein Fadhil al-Hulw ameandika makala kuhusu maudhui hii ambayo imechapishwa na tovuti ya Idara ya Mfawidhi wa Haram Ya Hadhrat Abbas (AS) maarufu. Hapa ni baadhi ya vipengee vya makala hiyo.
Watafiti wamepuuza sana umuhimu wa dua kama aina ya fasihi.
Dua na swala vina hadhi maalum katika sura ya kwanza ya Qur’ani Tukufu, Surah Al-Fatihah.
Katika marejeo ya kihistoria ya Qur’ani, pia kuna mtazamo maalum juu ya kuomba. Baada ya Adamu na Hawa kula tunda lililokatazwa, walimwomba Mwenyezi Mungu awasamehe:
“*Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika." (Aya ya 23 ya Surah Al-Aaraf)
Hii ni dua ya kwanza ya wanadamu. Sasa ni nani aliyewafundisha Adam na Hawa kuomba hivi na kutumia neno Rabb (Mola)? Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafundisha jinsi ya kuomba.
Ama neno Rabb au Mola, linaweza kuchukuliwa kuwa ni neno la kina ambalo ni dhihirisho la sifa zote za Mwenyezi Mungu: Uumbaji Wake, uwezo Wake, hekima Yake na rehema Yake.
Na jambo lingine muhimu ni kwamba hakuna dua yoyote katika Qur’ani inayoanza bila ya neno Rabb.
Mfano mwingine ni Aya ya 286 ya Surah Al-Baqarah:
“…(Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri..”
Marudio ya neno Rabb au Mola katika aya hii yanaashiria tumaini katika rehema ya Mungu na maonyesho ya utumwa kwa Mungu pamoja na dhihirisho la haja.
Katika Sura nyingine katika Qur’ani Tukufu, Nabii Ibrahim (AS) anakariri neno Rabb: “Mola, nijaalie mimi na dhuria wangu tuwe imara katika sala na ukubali ibada zetu. Mola Mlezi, Siku ya Kiyama, nisamehe mimi na wazazi wangu wawili na Waumini wote.”
Kwa hivyo uchunguzi wa aya za Qur’ani unaonyesha kuwa neno Rabb au Mola lina sifa maalum ambayo ni ya kipekee katika nyanja mbalimbali.
4233816