IQNA

Dua

Dua kwa Mwenyezi Mungu na mazingatio ya mwanadamu

21:57 - March 25, 2023
Habari ID: 3476759
TEHRAN (IQNA) – Dua inayosomwa wakati wa Suhur au daku katika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhamu inapaswa kumwinua mtu katika njia mbili: kwa upande mmoja inavuta mazingatio yake kwa Mungu na kwa upande mwingine haitamfanya apuuze matatizo ya jamii.

Haya ni kwa mujibu wa mwanachuoni wa Kiislamu Hujjatul Islam Mohammad Soroush Mahalati, akizungumza kuhusu umuhimu wa sala katika kikao cha kufasiri Dua ya Suhur. Hapa ni sehemu ya nukta za hotuba yake.

Lugha ya dua ni maalum si kwa sababu tu anayeombwa (Mwenyezi Mungu) ni tofauti na wengine ambao huombwa. Katika dua mtu huzungumza na Mwenyezi Mungu ambapo katika mazungumzo mengine, anazungumza na watu wengine.

Kuna tofauti nyingine kubwa hapa pia: Kwamba masuala ambayo yametajwa katika dua hayatajwi katika mazungumzo ya kawaida.

Dua zilizotufikia kutoka kwa Maasumin (AS) au Ahul Bayt wa Mtume Muhammad (SAW), kama vile Dua ya Kumayl, Abu Hamza Thumali, Shaabaniyah, Sahar, n.k, ni tofauti kwa sababu Maimamu Maasumin (AS) wanazungumza  njia tofauti wanapozungumza na watu wengine na wanapozungumza na Mwenyezi Mungu kwa njia ya  dua.

Tofauti ya kwanza ni kwamba katika dua hutajwa mafundisho yaliyo katika kiwango cha juu zaidi kuliko ya watu kwa ujumla. Kwa kawaida wanapozungumza na masahaba wao, Maimamu (AS) huzungumza katika kiwango cha mawazo na ufahamu wao lakini wanapozungumza na Mungu, hakuna kikomo kama hicho.

Ndio maana kuna nukta nyingi na mafunzo ya kina katika dua zilizosimuliwa kutoka kwa Maimamu Maasumin (AS) ambazo hazionekani katika Hadithi. Dua ya Sahar ni mojawapo ya dua hizi.

Tofauti ya pili ni kwamba katika lugha ya dua, Maimamu Maasumin (AS) pia hawakabiliwi na vikwazo vya kijamii na kisiasa. Ndio maana wanaashiria baadhi ya masuala ya kisiasa katika dua ambapo masuala hayo hayapatikani katika Hadithi.

Kwa mfano, kuna dua anayoisimulia Sheikh Tousi katika kitabu Al-Misbah al-Mujtahid inayosomwa katika Qunut na Sala ya Witr. Kuna falsafa ya kisiasa katika dua hii.

Kwa hivyo haipaswi kupuuza matatizo ya kijamii na kisiasa wakati wa dua kwa sababu tunazungumza na Mwenyezi Mungu wakati Sahar. Hata katika kukesha kila usiku akimwomba Mungu, muumini hapaswi kusahau jamii yake na matatizo kama njaa na umaskini ambayo watu wanakabiliana nayo.

4046515

captcha