IQNA

Turathi za Ahlul Bayt (AS)

Maandishi ya kale yanayofungamanishwa na Imam Hasan al-Askari (AS) yazinduliwa Mashhad

16:26 - September 11, 2024
Habari ID: 3479418
IQNA – Maandishi ya kale yanayonasibishwa na Imam Hasan al-Askari (AS) yamezinduliwa katika hafla katika Maktaba ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS) maarufu kama Astan Quds Razavi huko Mashhad, Iran.

Sherehe hizo zilifanyika Septemba 10, 2024, kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hasan al-Askari (AS).

Hafla hiyo ilifanyika katika chumba cha mikutano cha Maktaba Kuu ya Astan Quds Razavi, iliyohudhuriwa na mameneja na wataalamu kutoka maktaba, makumbusho na kumbukumbu za shirika.

Maktaba ya Astan Quds Razavi ina nakala 4,000 za 'Tafsiri ya Qur'ani' ikiwa ni pamoja na maandishi adimu yanaohusishwa na Imam Hasan al-Askari (AS).

Miongoni mwa hati 95 kama hizo katika maktaba kote nchini Iran, 26 zimehifadhiwa katika Maktaba ya Astan Quds Razavi, iliripoti tovuti ya shirika hilo.

Mohammad Vafadar Moradi, mtafiti na mtaalamu wa maandishi, alieleza kwamba maandishi hayo yana tafsiri yai hadi aya ya 282 ya Surah Al-Baqarah na yanajumuisha mijadala juu ya fadhila za Ahl al-Bayt (AS) miongoni mwa mada nyinginezo.

Moradi alibainisha kwamba Imam Hasan al-Askari (AS) aliishi chini ya miaka 30 na alikuwa amewekewa vizingiti na watawala huko Samarra wakati wa Uimamu wake. Pamoja na hayo, alitoa mchango mkubwa wa kielimu, alisisitiza mwanazuoni huyo.

Moja ya kazi zake mashuhuri, "Sahifa Askariya," ina sala na dua nyingi, ambazo ziliwasilishwa kwa masahaba zake na baadaye kuandikwa.

3489857

Habari zinazohusiana
Kishikizo: Imam askari
captcha