Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi, mkuu wa Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada, katika taarifa ya Jumamosi alimteua Majidimehr kuwa rais wa kamati hiyo.
Majidimehr ni msomaji mashuhuri wa Qur'ani na ana Shahada ya Uzamivu (PhD)katika Fiqh (sheria za Kiislamu).
Hapo awali amewahi kuwa mjumbe wa kamati za maandalizi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani ya Iran.
Mashindano ya 41 YA Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatarajiwa kufanyika katika mji mtakatifu wa kaskazini mashariki wa Mashhad mwanzoni mwa 2025.
Hafla hiyo ya kila mwaka inayoandaliwa na Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada ya Iran, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.
3490277