Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani la Iran limetangaza hatua ya mwisho siku ya Jumapili.
Kama ilivyo katika miaka iliyopita, mashindano yataanza kabla ya maadhimisho ya siku ya Kubaathiwa au kupewa Utume, Mtume Muhammad (SAW), ambayo mwaka huu itaangukia Januari 28.
Kulingana na tangazo hilo, hatua ya mwisho ya mashindano itafanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki wa kuanzia Januari 26 hadi 31.
Ukumbi wa Quds wa Taasisi ya Astan Quds Razavi utakuwa mwenyeji wa hafla ya ufunguzi.
Mashindano yatahitimishwa kwa hafla ya utoaji tuzo ambapo washindi wa juu katika kategoria mbalimbali. Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani la Iran. Yanalenga kukuza utamaduni wa Qur'ani na maadili miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani.
Mwaka huu, washiriki wanashindana katika aina za usomaji wa Qur'ani, Tarteel, na hifdhu ya Qur'ani Tukufu kwa wanaume na wanawake.
3491433