IQNA

Maadili ya Mtu Binafsi / Hatari za Ulimi 9

Kushuku ni mzizi wa tuhuma

21:30 - October 14, 2024
Habari ID: 3479595
IQNA - Asili ya Tuhmat au tuhuma kwa kawaida huwa ni dhann (kumshuku au kumdhania mtu vibaya). Kushuku tabia au maneno ya wengine kunaweza kusababisha mtu akatoa tuhuma iwe mbele ya mlengwa au akiwa hayupo.

Ilibainishwa hapo awali kuwa Tuhmat ni neno la Kiarabu linalotokana na mzizi Wahm na maana yake ni kutumka tuhuma mbaya iliyoingia moyoni.

Pia ilibainishwa kuwa Tuhuma au kuzua uongo ni miongoni mwa maovu ya kimaadili yaliyotajwa ndani ya Qur'ani Tukufu katika aya mbalimbali. Qur'ani kwa mfano inazungumzia jinsi makafiri walivyomtuhumu Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), kama vile Aya ya 21 ya Surah Al-Anam: “Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na akazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi.?

Aidha Katika Aya ya 12 ya Sura Hujurat tunasoma hivi: " Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi."

Kushuku au kuwa na dhana mbaya kuhusu wengine ni chimbuko la Tuhuma, ambayo inaweza kuwa ya aina mbili: Wakati mwingine mtu anahusisha tabia au hulka isiyofaa kwa mtu Fulani na hutoa tuhuma hizo mlwengi akwemo na  akiwemo na pili pia yamkini akatoa tuhuma hizo wakati mlengwa hayuko.

Muislamu sio tu kwamba hatakiwi kusikiliza Tuhma bali ajaribu kuzipinga. Kusema tu "usituhumu" haitoshi, kwa sababu sentensi hii yenyewe inaweza kuchukuliwa kama msisitizo juu ya uwepo wa dosari katika mtu ambaye anatuhumiwa.

Kuzuia ulimi kutuhumu kunahitaji juhudi za mara kwa mara. Tabaan, ifahamike kuwa siku hizo tuhuma si kwa njia ya ulimi tu bali katika zama hizo za teknolojia, pia mitandao ya kijamii, n.k inatumiwa kueneza tuhuma ima kwa mandishi au kwa klipu za video.

Dawa ya ugonjwa huu ni kuzingatia au kukumbuka matokeo yake mabaya. Kwa mujibu wa Qur'an Tukufu, “Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. (Aya ya 55 ya Surah Adh-Dhariyat)

Kukumbuka matokeo mabaya ya kueneza tuhuma kutafanya moyo wa mtu kuichukia na kumfanya mtu kuiacha. Mtu anapaswa pia kufikiria juu ya sifa ya wengine na kuwa mwangalifu asiichafue. Uislamu unaichukulia sifa ya waumini kuwa ni muhimu sana na hata baadhi ya riwaya zinasema ni muhimu Zaidi ya Kaaba tukufu. Mtu anayejua hili hatajiruhusu kamwe kukiuka utakatifu wa sifa ya wengine. Kuongezeka kwa Husn Dhann (kuwa na mawazo mazuri na chanya kuhusu wengine) pia ni tiba ya ugonjwa huu.

3490272

Kishikizo: maadili qurani tukufu
captcha