IQNA

Maadili ya Mtu Binafsi / Hatari za Ulimi 7

Kusengenya ni dhambi kubwa katika Uislamu

22:09 - October 08, 2024
Habari ID: 3479563
IQNA - Buhtan (kusema uongo, kusingizia na pia kusengenya), ni kitendo ambacho hutendwa kwa ulimi n.k ili kuharibu sifa ya mtu na huchukuliwa kuwa ni dhambi kubwa katika Uislamu.

 Kusengenya ni dhambi kubwa katika UislamuKulingana na wasomi wa maadili, inamaanisha kumhusisha mtu kwa uwongo na tabia au taarifa isiyofaa.
Buhtan ni kitendo kisichofaa ambacho wakati mwingine hujulikana kama tawi la kusengenya.
Kwa Kiarabu, Buhtan asili yake ina maana ya kustaajabishwa au kumshangaza mtu. Hutumika kueleza kitendo cha kusema mambo kuhusu mtu ambayo si ya kweli na hivyo kusababisha mshangao. Wakati mwingine maneno matatu Butan, Tuhmat na Iftiraa hutumiwa kurejelea kitu kimoja, ingawa yanatofautiana kimsamiati na kiistilahi. Buhtan maana yake ni kuhusisha au kunasibisha kitu kwa uwongo na mtu fulani, wakati Iftiraa maana yake ni kuzusha au kutunga uwongo na Tuhmat maana yake ni tuhuma.
Kuna Hadithi nyingi zinazoonya dhidi ya Buhtan. Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr Ghaffari ambaye alimuuliza Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) Je, Ghibah (kusengenya) ni nini? Mtume (SAW) alijibu kwa kusema ina maana ya kuzungumzia mapungufu au nuksani za ndugu yako katika imani ambayo hapendi kuongelewa. Abu Dharr aliuliza , je ni vipi kiwa mtu huyo ana sifa ambazo zinanasibishwa naye. Mtume (SAW) alisema kama ana upungufu huo umetenda Ghibah na kama hana umefanya Buhtan.
Buhtan ni ya aina mbili. Wakati mwingine tabia isiyofaa inahusishwa kwa uwongo na mtu kwa kutokuwepo kwake. Aina hii ya Buhtan inahusisha dhambi mbili kubwa: kusema uwongo na kusengenya. Aina nyingine ya Buhtan ni wakati mtu anahusishwa na kitu kwa uwongo  mbele yake.
Buhtan ni miongoni mwa madhambi ya ulimi na bila shaka dhambi hii imeharamishwa katika Uislamu. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 58 ya Surah Al-Ahzab: “Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa (buhtan) na dhambi zilio dhaahiri.
Aya hii inataja Buhtan kuwa ni dhambi iliyo wazi na kubwa. Katika Hadithi mbalimbali, Buhtan inaelezewa kuwa ni dhambi ambayo itampeleka mtu kwenye moto wa Jahanam. Kwa mujibu wa Hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), yeyote ambaye kwa uwongo ananasibisha jambo fulani kwa Muumini mwanamume au mwanamke, Mwenyezi Mungu atamweka juu ya rundo la moto mpaka aondokane na yale aliyoyasema.
3490181

captcha