IQNA

Maadili ya Mtu Binafsi / Hatari za Ulimi 10

Je! ni aina gani ya jidal imeidhinishwa na Qur'ani?

20:38 - October 17, 2024
Habari ID: 3479607
IQNA - Jidal, katika maadili, inahusu kubishana na katika hali mbaya ya idal, mtu hubishana ili hatimaye aonekana ndie mwenye kuibuka mshindi.

Uislamu hauzingatii tu masuala ya kibinafsi ya mwanadamu bali pia mahusiano yake ya kijamii. Katika Uislamu, jinsi ya kuingiliana na wengine kwa maneno na vinginevyo ni muhimu sana. Ukweli, uaminifu, tabia njema na mengine yanayofanana na hayo ni maadili mema ambayo yamesisitizwa katika Uislamu huku ikikataza maovu ya kimaadili kama kusema uwongo, kutokuwa mwaminifu, kukashifu n.k.
Jidal pia wakati mwingine hukatazwa sana katika Uislamu wakati inapojidhihirisha kama  kama ugonjwa wa ulimi ambao unahitaji kuponywa.
Katika maadili, Jidal inarejelea kugombana vikali na mtu ili kumshinda. Jidal kama hii inaweza kuwa na lengo la kuongoza mtu katija njia ya haki kinyume na ile Jidal yenye malengo ya kibinafsi au yenye kuelekea katika malengo maovu.
Ikiwa lengo ni ovu, mtu anajaribu kupata ubingwa dhidi ya mtu mwingine katika mabishano ili kupata cheo au mali, nk Ikiwa lengo ni takatifu, mtu anajaribu kumwongoza mtu ambaye ni mjinga.
Suala la Jidal limetajwa katika aya za Quran kwa namna mbili. Baadhi ya aya hazikubaliani na Jidal, kama Aya ya 4 ya Surah Ghaafir: “Hawazibishi Ishara za Mwenyezi Mungu ila walio kufuru…”
Baadhi ya aya nyingine zimeidhinisha na hata kumuamrisha Jidal, kama Aya ya 125 ya Surah An-Nahl: “Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora...”
Mtu anaweza kufikiri kwamba kuna mgongano kati ya aya mbili hizo, lakini uchunguzi wa makini juu yao unaonyesha kwamba Quran inaikataa aina ya Jidal ambayo ina makusudio maovu, lakini inaidhinisha Jidal kwa makusudio ya kumfikia Mwenyezi Mungu.
Jidal ambayo inakataliwa na Qur’ani ina mizizi katika sifa mbaya ndani. Chanzo cha Jidal hii ni sifa kama vile hasira, kupenda dunia, na majivuno.
Ina matokeo mabaya kama vile kusababisha unafiki, uwongo na uadui. Mtu anayeingia Jidal bila ya kuwa na uwezo wa kutosha kwa hilo anaweza kuamua kusema uwongo ili kutetea hoja yake na wakati mwingine anaweza kumwambia mwenzake kuwa yuko sahihi kwa unafiki tu.
Kuna njia mbili za kutibu Jidal ambayo inakataliwa na hekima na dini. Moja ni kukumbuka matokeo yake mabaya na nyingine ni kuwaheshimu wengine.
 3490288

Kishikizo: maadili qurani tukufu
captcha