Uislamu haukubaliani na tabia hiyo hata kidogo, kiasi kwamba Qur’ani Tukufu inawaamuru Waislamu hata wasitukane miungu ya makafiri.
Kutukana kunaweza kugawanywa katika aina kadhaa kwa kutegemea nia ya mwene kutukana.
Wakati mwingine hutumiwa kuudhi mtu, ambapo mtu anayetukana anadharau sifa ya mtu mwingine. Wakati fulani kutukana au kutusi huwa kwa ajili ya kujifurahisha tu. Na katika baadhi ya matukio, tabia hii isiyofaa huwa inatokana na mazoea na bila nia maalum.
Vyovyote vile nia, kitendo cha kutukana na kutusi kimekatazwa na Uislamu, kiasi kwamba Qur’ani Tufu inakataza hata kutukana miungu ya makafiri: Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua...” (Aya ya 108 ya Surah al-Anaam)
Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ambaye amesema kulaani na kuapa hakuna nafasi katika Uislamu.
Kutukana hupanda mbegu za uadui na chuki katika mioyo ya wengine. Mtu anayewatukana wengine huongeza tu adui zake badala ya kueneza urafiki.
Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amesema: “Usiwatukane wengine usije ukawafanya wawe maadui wako.
Matokeo mengine ya kutukana ni pamoja na kupunguzwa riziki, dua kutojibiwa, kupoteza janna, na kuingia motoni. Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kwamba kuingia peponi ni Haramu kwa wale wanaotukana
Ili kuondokana na ugonjwa huu wa maadili, mtu anapaswa kujaribu kukabiliana na sababu zake za mizizi, kama vile hasira. Kujitahidi kuzungumza lugha nzuri na maneno sahihi ni njia mojawapo ya kutibu maradhi ya hulka mbaya ya kupenda kutukana. Kuzoea maneno mazuri husaidia kuondoa tabia ya kutumia maneno mabaya.
3490334