Kwa hivyo Istihza ina vipengele viwili: 1- Kuiga wengine 2- Kuwa na nia ya kuwachekesha wengine.
Istihza ni miongoni mwa tabia zisizofaa ambazo baadhi ya watu huzitumia kuwadhalilisha wengine. Ni miongoni mwa maradhi kuu yasiyofaa ya ulimi ambayo yana athari mbaya, kama vile kuwakasirisha watu, kujenga uadui, na kuibua hisia ya kulipiza kisasi. Pia huharibu roho ya umoja na mshikamano katika jamii ya wanadamu.
Istihza ni kukiuka sifa za watu wengine na kuwadharau. Qur'ani Tukufu inakataza kitendo hiki waziwazi. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 11 ya Surah Al-Hujurat: "Enyi Waumini, wanaume wasiwacheke wanaume wenzao. Wala wanawake wasiwadhihaki wanawake ambao wanaweza kuwa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu."
Tunasoma katika Aya ya 49 ya Surah Al-Kahf: “Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.”
Ama kuhusu ibara ya “Hakuna dogo wala kubwa”, Ibn Abbas amesimulia Hadithi ambayo dogo hapa linahusu kutabasamu wakati Muumini anapofanyiwa mzaha na kubwa inahusu kucheka wakati Muumini anafanyiwa mzaha.
Ikiwa Istihza inafanywa wakati mtu hayupo na inahusu kasoro zilizofichika za mtu, pia inachukuliwa kuwa ni Ghibah (kusengenya), ambayo ndiyo inayoitwa dhambi dhambi.
Ili kutibu ugonjwa huu, mtu anapaswa kutafakari juu ya matokeo yake mabaya. Istihza inajenga uadui hapa duniani na inaleta adhabu huko akhera.
Istihzai humdhalilisha mtu mwingine na kumshushia hadhi, na mwenye kufanya istihzai anaweza kufanyiwa jambo lile lile analomfanyia mzaha mtu mwingine.
Kwa mujibu wa maelezo ya kihistoria, baba yake Marwan alikuwa akimfuata Mtukufu Mtume Muhammad (SAW.) na kudhihaki jinsi alivyotembea. Siku moja Mtume (SAW.) alimuona na akaomba abaki katika hali ile ile aliyokuwa nayo. Baba yake Marwan alipatwa na Ugonjwa wa Parkisnon hadi akafa.
Wale wanaodhihaki wengine wanapaswa kufikiria jinsi wangehisi ikiwa wangedhihakiwa. Kwa kutafakari mambo haya, inatumainiwa kwamba mtu huyo ataacha kuwadhihaki wengine na kutafuta njia ya kuponya ugonjwa huo alionao kwa kuwafnayia wengine istihzai.
3490305