Kwa mujibu wa maadili ya Kiislamu, tabia hii ina madhara mengi mabaya kama vile kupoteza wakati katika maisha, udhalilishaji katika jamii, kueneza dhambi za ulimi kama vile kusema uwongo, kashfa na kusengenya, kujiepusha na rehema za Mwenyezi Mungu, kukosa muda wa kufanya mambo yenye manufaa, kupotoka, kudhoofisha uwezo wa kakili, nk.
Kuna aina nyingi za mazungumzo ya kipuuzi, kuanzia kuzungumza juu ya mada zisizo na maana hadi kutoa kauli zisizo na maana, kuuliza maswali yasiyofaa na kutoa hoja tata au nadharia kwa wale ambao hawaelewi.
Kwa mtazamo wa kimantiki, mazungumzo ya kipuuzi yanaweza kutajwa kuwa ni haramu kwa sababu yanapoteza muda wa maisha ya mtu, muda ambao ni mali au rasilimali yake muhimu zaidi. Hadithi pia zinaunga mkono mtazamoa huu wa kimantiki.
Mtume Muhammad (SAW) amesema katika Hadith ya Mi’raj kwamba kuna milango saba katika Jahannam, ambayo kila moja imeandikwa sentensi tatu, na kwenye mlango wa tano imeandikwa: “Msizungumze yasiyo na maana, kwani mtakosa rehema za Mungu.”
Kwa mujibu wa Hadithi nyingine kutoka kwa Mtukufu Mtume (SAW.), moja ya mambo mazuri ndani ya mtu ni kuacha yale ambayo hayana faida.
Mtume Muhammad (SAW) pia alimshauri Abu Dharr al-Ghifari kushikamana na ukimya, tabia njema na kuepuka shughuli zisizo na maana.
Wataalamu wa maadili wametaja sababu nyingi kwa nini watu huwa na tabia ya kuzungumza mambo yasiyo na maana wala muelekeo. Baadhi ya sababu hizi ni pamoja na udadisi usiofaa, kutumia muda mwingi na wengine, kujaribu kuvutia usikivu wa wengine, na kupenda umaarufu.
Mojawapo ya mikakati bora ya kuzuia mazungumzo yasiyo na faida ni kutafakari juu ya thamani ya maisha ya mtu. Mtu anapaswa kutambua kwamba wakati wenye thamani anaotumia kuzungumza juu ya mambo yasiyofaa hautapatikana tena, na atapoteza fursa nyingi maishani ambazo zingeweza kutumika katika kujistawisha na kujiboresha.
3489883