Kuna wale wenye tabia ya kumkejeli mtu aliyepatwa na msiba au masaibu kwa dhana potofu kuwa yeye ndiye aliyejisababishia yaliyomsibu.
Kuna aina mbili za kufurahia masaibu ya wengine: batini na Dhahiri. Katika aina ya kwanza, tunahisi furaha mioyoni mwetu kwa bahati mbaya ya wengine, lakini hatuonyeshi furaha yetu. Katika aina ya pili, hata hivyo, tunaonyesha furaha yetu na kumkemea au kumkejeli mtu, kumwambia kwamba masaibu aliyomfikia ni matokeo ya mwenendo wake.
Wakati mwingine tabia iliyosababisha masaibu sio mbaya kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyekumbwa na masaibu. Kwa mfano, mtu akionyesha ukarimu, bakhili huona kuwa haifai, na mkarimu akipatwa na matatizo kwa sababu ya ukarimu wake, bakhili hufurahi na kumlaumu.
Huu ni mfano wa wazi wa namna wanafiki wanavyofurahia masaibu ya waumini. Aina ya pili ni pale mtu anakumbwa na masaibu kutokana na kuacha mafundisho ya kidini. Kwa ujumla kufurahia maafa ya wengine ni jambo linalochukizi kidini na hata kimantiki. Akili ya mwanadamu na Fitra (asili), kwa mujibu wa asili yake ya kijamii, huwatakia wengine mema na kwa msingi huo kufurahia masaibu ya wengine ni kinyume cha maumbili ya mwanadamu.
Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na Maimamu Maasumin (AS) wameonya dhidi ya tabia hiyo katika Hadith nyingi. Mtume Muhammad (SAW) alisema usimlaumu ndugu yako (na ufurahie msiba wake) kwa sababu Mwenyezi Mungu anaweza kukusababishia msiba huo huo.
Pia, Imamu Sadiq (AS) alisema mtu anayemlaumu ndugu yake katika imani kwa msiba uliompata hataondoka duniani mpaka yeye mwenyewe apatwe na msiba huo huo.
Kufurahia bahati mbaya ya wengine haifai kwa namna yoyote, iwe furaha hiyo ni dhahiri na ya wazi au batini na iliyojificha moyoni.
Kufurahia masaibu ya wengine hutokana na hasira isiyozuilika. Wakati hasira isipodhibitiwa na akili, husababisha maovu kama vile uadui na husuda, ambayo huleta tabia mbovu ya kufurahia masaibu ya wengine.
Anayejishughulisha na tabia hii anaweza kukumbana na balaa hapa duniani na adhabu kesho akhera. Ili kuponya ugonjwa huu wa maadili, mtu anapaswa kutafakari juu ya matokeo yake na kukumbuka daima kwamba anaweza kupata bahati mbaya ambayo mwingine ameipata. Vile vile anapaswa kuzingatia kwamba masaibu wanayopata waumini yanaweza kuwa yenye lengo la kuwasamehe dhambi zao au kuwaleta karibu na ukamilifu huko akhera. Kutambua hilo kutamsaidia kuacha kufurahia madhambi ya wengine.
3489910