Wakati mwingine makusudio ya Khusuma ni kufikia lengo la kifedha au haki. Mzozo kama huo wakati mwingine hufanywa ili kuthibitisha maoni ya mtu, na hiyo inaweza pia kuzingatiwa kama aina ya kurejesha haki.
Khusuma wakati fulani ni ugonjwa wa ulimi unaoweza kusababisha uadui na kusambaratika kwa jamii ya wanadamu.
Kwa hivyo, sio kila khusuma inachukuliwa kuwa tabia mbaya au hasi. Wanachuoni wa maadili wanagawanya Khusuma katika aina mbili: Ya kusifiwa na isiyokubalika. Akili na dini zinasifu baadhi ya aina za Khusuma na kuzikataa baadhi ya aina nyingine.
Khusuma inakubalika ikiwa tu mtu ana yakini juu ya uhalali wake au ana uthibitisho wa kidini juu yake na haoni njia nyingine ya kurejesha haki yake.
Kwa kuwa dhulma haifai, akili ya mwanadamu inaona kuwa si sawa kukubali dhulma, hivyo akili ya mwanadamu inasifu kukabiliana na dhulma, na ikiwa hakuna njia nyingine zaidi ya Khusuma kurejesha haki, akili ya mwanadamu huisifu na kuipendekeza, na bila shaka Uislamu unaafiki msimamo sahihi wa kutetea haki.
Wale ambao hawana uhakika kuhusu iwapo wako katika au la au iwapo wana yakini kuwa hawaka katika haki hawapasi kujihusisha na Khusama. Hii ni kwa sababu Khusuma kama hiyo inachukuliwa kuwa mojawapo ya sifa za nguvu ya hasira.
Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amesema kwamba mtu anayechukiwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni mtu mgumu zaidi, mgomvi.
Mtume (SAW) pia alisema kwamba ikiwa mtu ataonyesha ukaidi katika Khusuma bila ya kuwa na yakini kuwa yuko sahihi, hukabiliana na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu maadamu yuko katika hali hiyo.
Baadhi ya mizizi ya Khusuma isiyokubalika ni pamoja na kutojali, wivu, na kupenda mali au cheo. Njia ya vitendo ya kutibu ugonjwa huu ni kutumia kinyume chake, ambacho ni Teeb wa Kalam.
Teeb Al Kalam inamaanisha kutumia maneno mazuri na ya adabu. Mtu anapaswa kujitolea kuwa Teeb Al Kalam, yaani, anapaswa kujitahidi kubaki mwenye adabu na kutumia maneno yanayofaa na mazuri anapozungumza na mtu mwingine.
Kama vile Khusuma, Maraa, na Mujadilah hujenga uadui, kinyume chao, Teeb Al Kalam, hujenga urafiki na usuhuba. Wengine wanapoona kwamba mtu yuko makini katika mambo anayosema, wanavutiwa naye. Sifa hii ikiwa imeenea katika jamii, huleta umoja na maelewano, tofauti na Khusuma ambayo husababisha mfarakano na migongano.
3489998