Aina moja ya umbeya ni ile ambayo kwa Kiarabu inajulikana kama Namimah ambayo tunaweza kusema ni kumwambia mtu kwamba mtu mwingine amezungumza kukuhusu na kusema hili na lile kukuhusu.
Aina nyingine yake ni ule umbeya kwa wafalme na watawala ambao kutoka kwao mtu anahisi kutishiwa kufungwa, kufukuzwa, au kuuawa.
Qur'ani Tukufu inaonya vikali dhidi umbeya. Katika Aya ya 1 ya Surah Humazah, Mwenyezi Mungu anasema, " Ole wake kila safihi, msengenyaji!"
Katika Surah Al-Qalam, Aya ya 10-12, Allah SWT anamwambia Mtukufu Mtume: “Wala usimt´ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa. Mtapitapi, apitaye akifitini. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi.
Kwa mujibu wa Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), wazushi ni miongoni mwa watu wabaya zaidi.
Mtu ana majukumu kadhaa mbele ya wenye uzushi na wanaoeneza umbeya. Kwanza, asithibitishe wanachosema kwa sababu wao ni watenda dhambi na ushuhuda wao si halali.
Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 6 ya Surah Al-Hujurat: Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda".
Pili, Mwenyezi Mungu amewaonya dhidi ya ngano, ambayo ni miongoni mwa dhambi na matendo maovu. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 17 ya Sura Luqman: “Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli."
Tatu, mtu anapaswa kukaa mbali na wazushi, ambao Mwenyezi Mungu hawapendi. Nne, Mtu asiwe na mawazo mabaya na mashaka juu ya mtu ambaye wazushi humsema vibaya.
Nne, Kwa mujibu wa Aya ya 12 ya Surah Al-Hujurat, Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi..."
Na tano Aya ya 12 ya Surah Al-Hujurat: "… Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu."
/3490356