IQNA

Maadili ya Mtu Binafsi / Hatari za Ulimi 8

Kusingizia uongo huwa na matokeo hasi kwa watu binafsi, Jamii

22:04 - October 12, 2024
Habari ID: 3479582
IQNA - Buhtan (kusingizia uongo na pia kusengenya), yaani kutoa taarifa ya uwongo inayoharibu sifa ya mtu, huwa na matokeo mabaya kwa mtu binafsi na jamii.

Mtu anayejihusisha na Buhtan hatimaye atafedheheshwa. Mtu kama huyo hupoteza sifa yake katika jamii.
Buhtan ni miongoni mwa madhambi ya ulimi na bila shaka dhambi hii imeharamishwa katika Uislamu. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 58 ya Surah Al-Ahzab: “Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa (buhtan) na dhambi zilio dhaahiri.
Buhtan ni matokeo ya sifa mbaya za dhati ya mtu.
Kusingizia uongo hutokana na tabia na sifa mbaya ya mtu binafsi na iliyokita mizizi kama vile:
1- Uhasama. Nyakati nyingine mtu husema kwa uwongo na mambo yasiyofaa kuhusu mtu mwingine kutokana na chuki alizonazo.
2- Wivu. Wakati mwingine mtu huhisi wivu kutokana na hali bora ya mtu mwingine au mafanikio yake na hukimbilia uenezaji uongo ili kumdhoofisha.
3- Hofu na hamu ya kukwepa adhabu. Wakati mwingine mtu huogopa kuadhibiwa kwa kosa, au anataka kuzuia kosa lisihusishwa naye, na kwa hivyo hukimbilia uenezaji uzushi na uongo kuhusu wengine.
Matokeo mabaya ya buhtan ni makali zaidi kuliko yale ya ghibah (kusengenya), kwa sababu katika ghiba hutajwa hutajwa dosari ambazo ziko kwa mtu mwingine, wakati katika katika buhtan uongo na uzushi huenezwa kuhusu mtu mwingine.
Buhtan ina matokeo mabaya mengi kwa mtu binafsi na jamii.
Inapanda mbegu za uadui na chuki katika jamii na kugeuza urafiki kuwa uadui. Buhtan huharibu hisia ya uaminifu, ambayo ni msingi wa malezi ya vitengo vidogo na vikubwa katika jamii.
Inaweza kuathiri vibaya uhusiano wote, kugeuza ndoa kuwa talaka, kudhoofisha uhusiano kati ya baba na wana, na hata kusababisha uhalifu kama vile mauaji.
Imepokewa kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kwamba yeyote ambaye kwa uwongo ananasibisha jambo fulani kwa Muumini mwanamume au mwanamke, Mwenyezi Mungu atamweka juu ya rundo la moto mpaka aondokane na yale aliyoyasema.

3490195

Kishikizo: maadili qurani tukufu
captcha