IQNA

Qarii Mashuhuri

Qiraa ya Qur'ani ya Mustafa Ismail: Chanzo cha Msukumo kwa Vizazi

20:16 - December 29, 2024
Habari ID: 3479970
IQNA – Wizara ya Wakfu ya Misri imemuenzi qari maarufu Sheikh Mustafa Ismail katika kumbukumbu ya kifo chake.

Wizara ilisema kwenye tovuti yake rasmi kwamba qiraa yake ya Qur'ani ni chanzo cha msukumo kwa vizazi vijavyo.

Aliacha urithi usio na kifani wa ukariri unaoakisi uzuri wa sauti na Maqamat (mbinu za qiraa), ilisema. Wizara ilionyesha kipaji cha kipekee cha Sheikh Mustafa Ismail katika kuchanganya sheria za Tajweed na sayansi ya qiraa na sauti.

Ilisema kwamba qari huyo mashuhuri aliweza kuwasilisha ukubwa wa dhana za Qur'ani kwa mioyo ya wasikilizaji wake, na kumfanya kuwa mmoja wa wavumbuzi katika qiraa. Wizara iliwataka wote kusikiliza qiraa za Sheikh Mustafa Ismail, ambazo zinasikika kwenye Idhaa ya Qur'ani kama mfano wa uvumbuzi na athari ya kiroho.

Wizara pia ilisisitiza kwamba kumbukumbu ya Sheikh Mustafa Ismail inabaki hai katika jamii ya Waislamu, ikimtambua kama shakhsia wa kipekee wa Qur'ani ambaye alitajirisha sana urithi wa qiraa na ubunifu wa Qur'ani.

Sheikh Mustafa Ismail alikuwa qari ambaye alianzisha mtindo mpya wa qiraa ambapo aliweza kwa namna fulani kuelezea dhana za aya kupitia sauti yake nzuri. Alizaliwa Juni 17, 1905, katika kijiji kinachoitwa Mit Gazal karibu na mji wa Tanta katika Jimbo la Gharbia la Misri.

Wazazi wake walimwita Mustafa Muhammad Mursi Ismail. Baba yake, ambaye alikuwa mkulima, alimpeleka kwenye shule ya Qur'an iliyoongozwa na Sheikh Abdul Rahman Abulainain kuhifadhi Qur'ani. Mustafa Ismail aliweza kujifunza Quran nzima kwa moyo akiwa na umri wa miaka 10.

Kisha akaanza kujifunza qiraa ya Qur'ani na kanuni za Tajweed na Sheikh Idris Fakhir. Kwa mara ya kwanza alisoma Qur'ani mbele ya umati akiwa na umri wa miaka 14. Wale waliomsikia akisoma katika Msikiti wa Atif huko Tanta walishangazwa na qiraa yake nzuri na kumhimiza aendelee na njia ya qiraa ya Qur'ani. Alifanya hivyo kwa kwenda Cairo na kujifunza zaidi katika uwanja huo kutoka kwa Qari mashuhuri Sheikh Muhammad Rafa’at.

Alijulikana sana kote Misri na alisafiri kwenda nchi nyingi, zikiwemo Iraq, Indonesia, Saudi Arabia, Pakistan, Ujerumani, Palestina, Uingereza na Ufaransa kusoma Qur'ani katika vikao mbali mbali.

Pia alipokea medali nyingi za heshima nchini mwake na kwingineko. Sheikh Mustafa Ismail aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake Desemba 26, 1978 na alizikwa nyumbani kwake. Hapa chini ni moja ya qiraa yake ya Qur'ani:

3491243

captcha