Wanachama wa jopo la majaji wa mashindano hayo walihudhuria semina hiyo.
Iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Dini na Awqaf ya Algeria chini ya usimamizi wa Waziri wa Awqaf, Youssef Belmehdi, kulingana na ripoti ya tovuti ya radioalgerie.
Katika semina hiyo, Tahir bin al-Ghuni Idris Na’im Al-Muhasibi, mtaalam kutoka Nigeria na mwanachama wa jopo la majaji, alitoa mhadhara wenye kichwa “Fadhila za Qur’ani na Heshima ya Kuihifadhi na Kuifuata”.
Youssef bin Muslih bin Mahl Al-Raddadi, mwanachama kutoka Saudi Arabia wa jopo hilo, alizungumzia mada ya mitindo ya kisomo cha Qur’ani katika historia na katika zama za kisasa.
Katika hotuba yake, Waziri Belmehdi alisema kuwa kuandaa programu za kielimu na kifikra kama hizi ni shughuli ya ziada kwa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani nchini Algeria, yenye lengo la kunufaika na uzoefu wa wanachama wa kamati ya majaji.
Pia alisisitiza juhudi za Algeria katika kuhudumia Qur’ani Tukufu.
Raundi ya mwisho ya Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Algeria ilianza katika hafla ya ufunguzi jijini Algiers siku ya Jumanne.
Mashindano hayo yanahitimishwa leo, Januari 25, na washindi wa juu watatunukiwa tuzo katika hafla ya kufunga itakayofanyika Januari 26.
Miongoni mwa waliotinga fainali ni mhifadhi wa Qur’ani mzima kutoka Iran, Ali Gholamazad.