Khaled Meshaal, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas nje ya Gaza, alitoa kauli hiyo katika hafla iliyofanyika Cairo ya kuwaenzi wafungwa wa Kipalestina waliokombolewa hivi karibuni kutoka magereza ya utawala katili wa Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel.
Alisema kuwa operesheni hiyo, iliyofanywa na wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS dhidi ya utawala wa Israel mnamo Oktoba 7, 2023, iliunda dhoruba kubwa yenye faida kuu za kistratejia.
"Tutaona athari za dhoruba hii, na tumeona jinsi utawala wa Kizayuni unavyoanguka kutoka ndani na majeraha yake yanavyozidi kuwa makubwa. Tutaona jinsi dhoruba hii inavyofichua sura mbaya ya utawala wa Israel kwa dunia na kufanya propaganda zake za upotoshaji kuwa batili baada ya miongo kadhaa."
Pia alitoa wito wa umoja wa kitaifa Palestina kwa misingi ya kanuni, akiongeza kuwa Palestina itapata msaada zaidi katika ngazi ya kikanda na kimataifa.
wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, ulitekeleza Operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa kama jibu kwa miongo kadhaa ya utawala huo katili wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na maeneo yao matakatifu.