Katika taarifa yao, Rashida Tlaib (D-Mich.), Ilhan Omar (D-Minn.), André Carson (D-Ind.), na Lateefah Simon (D-Calif.) walisema:
“Matusi haya ya kuchukiza, ya kibaguzi na ya chuki dhidi ya Uislamu kutoka kwa wenzetu wa vyama vyote viwili dhidi ya Zohran Mamdani hayawezi kufumbiwa macho.”
Zohran Mamdani, mwanasiasa wa mrengo wa chama che Democrat mwenye misimamo ya kijamaa, anaweza kuwa Muislamu wa kwanza kuwa meya wa jiji kubwa zaidi nchini humo iwapo atashinda uchaguzi mkuu wa Novemba. Hata hivyo, amekuwa akishambuliwa na Warepublican akiwemo Andy Ogles wa Tennessee, ambaye aliiomba rasmi serikali ya Marekani imnyang’anye uraia na kumfukuza nchini.
Mbunge mwingine, Nancy Mace (R-S.C.), alichapisha picha ya Mamdani akiwa amevaa kanzu na kuandika, “Baada ya 9/11 tulisema ‘Tusisahau.’ Kwa kusikitisha, inaonekana tumesahau.”
Wabunge Waislamu walionesha masikitiko kuwa hakuna hata mmoja wa Wademocrat kutoka New York aliyelaani wazi matamshi hayo ya chuki. Kinyume chake, Seneta Kirsten Gillibrand (D-N.Y.) alimshutumu Mamdani kwa madai ya uongo kwamba aliwahi kutamka kuhusu “jihad ya kimataifa” na kwamba kauli ya “kueneza intifada kimataifa” ni mwito wa “kuua Wayahudi wote.”
Mbunge mpya, Lauren Gillen (D-N.Y.), pia alimlaumu Mamdani kwa kile alichodai ni “mwenendo wa kutisha wa maoni ya chuki dhidi ya Wayahudi.”
Katika taarifa yao, wabunge Waislamu waliongeza:
“Tunaifahamu vizuri lugha hii ya chuki, kwani tumekuwa wahanga wake mara nyingi.”
Ilhan Omar na Rashida Tlaib wamekuwa wakilengwa na mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu na vitisho vya kuuawa kwa miaka mingi , kutokana na asili zao kama mkimbizi mwenye asili ya Somalia na Mpalestina-Mmarekani.
Kama Mamdani, wao pia wamekosolewa kwa kuunga mkono uhuru wa Palestina na kupinga uvamizi wa Israel, ukaliaji wa mabavu, ukoloni, na mfumo wa ubaguzi wa rangi dhidi ya Wapalestina — mambo yanayoshughulikiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kama kesi ya mauaji ya halaiki.
Tangu Oktoba 7, 2023 , wakati utawala wa Israel ulipoanzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza, mashirika ya haki za binadamu yameripoti ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu na Wapalestina, hali inayofanana na ile ya baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001.
“Katika kipindi hiki cha ongezeko la vurugu dhidi ya viongozi waliochaguliwa, hatuwezi kuruhusu mashambulizi dhidi ya Zohran Mamdani yaendelee,” wabunge hao walisisitiza. “Mashambulizi haya huchochea kuendelea kwa ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu wa Marekani. Tunayakataa vikali.”
Mbunge Pramila Jayapal (D-Wash.) pia alitoa tamko la kulaani “wimbi la kauli za chuki, hatari na kibaguzi kutoka kwa baadhi ya wabunge na maafisa wa zamani wa utawala wa Trump.”
Jayapal alisema:
“Kumuita Mamdani raia wa Marekani awe denaturalized na kufukuzwa ni jambo la aibu na ni kinyume cha sheria za nchi hii.” “Lugha hii ya chuki inaweza kusababisha mtu kuuawa. Lazima tukemee waziwazi. Kila anayejali demokrasia, uhuru wa dini, na haki ya kila Mmarekani kutendewa kwa usawa, lazima asimame na kusema: Inatosha!”
3493617