IQNA

Ushirikiano katika Qur’ani Tukufu/4

Misingi ya Nadharia ya Ushirikiano na Usalama wa Kijamii

17:38 - October 21, 2025
Habari ID: 3481395
IQNA – Ushirikiano na usalama wa kijamii kwa wale waliotengwa na wahitaji ni miongoni mwa masharti muhimu ya mwenendo wa waumini, kwa mujibu wa aya za Qur’ani Tukufu na Hadithi za Ahlul-Bayt (AS).

Katika Surah Al-Muddaththir, Qur’ani inasimulia mazungumzo baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni, ambapo moja ya sababu za kuingia Motoni ni kutowalisha wahitaji:

“‘Ni nini kilichokusukuma kuingia katika Moto mkali?’ Watajibu: ‘Sisi hatukuwa miongoni mwa wanaoswali, wala hatukuwalisha wahitaji. Tulijitumbukiza na wanaojitumbukiza, na tukakanusha Siku ya Malipo.’” (Aya 42–46)

Suala hili halihusiani tu na Akhera. Katika Surah Al-Fajr, miongoni mwa sababu za kudhalilika kwa watu na kutengwa na rehema ya Mwenyezi Mungu hapa duniani ni kutowaheshimu mayatima na kutokuhamasishana kuwalisha masikini:

“Lakini Mola wake anapomjaribu kwa kumpa riziki kwa kipimo, husema: ‘Mwenyezi Mungu amenidhalilisha.’ (Kwa kuwa mali si dhamana ya furaha ya kudumu) basi kwa nini hamuwatendei wema mayatima, wala hamuhimizani kuwalisha wahitaji?” (Aya 16–18)

Kuna mambo kadhaa yaliyofichika katika kauli “kuwatendea wema mayatima”: Kwanza, kilicho muhimu zaidi kuliko mwili wa yatima ni roho yake, ambayo inapaswa kuheshimiwa. Kwa maneno mengine, matarajio ya kwanza ya mayatima ni heshima ya utu wao. Kuheshimiwa kwa mwanadamu na Mwenyezi Mungu kunapaswa kupelekea kuheshimiwa kwa mayatima.

Kauli “kuhimizana” pia ina maana ya kuhamasishana. Hii inaonesha kuwa kuwalisha masikini pekee haitoshi, bali ni lazima kuhamasishana na kushirikiana katika hilo.

Kwa hivyo, ushirikiano una nafasi muhimu katika kuwaheshimu mayatima, kuwatendea wema wahitaji, na katika kuhakikisha riziki na heshima ya kibinadamu.

Mbali na kusisitiza usaidizi wa pamoja katika kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi ya masikini na waliotengwa, Qur’ani na Sunnah zinataja misingi ya kifalsafa kama vile: mali ni ya jamii, imani katika haki ya kila mtu kwa utajiri wa asili, udugu wa Kiislamu, na ushiriki wa masikini katika mali ya matajiri.

Katika maelezo yanayofuata, baadhi ya misingi ya ushirikiano itatajwa.

/3495043/

Kishikizo: qurani tukufu jamii
captcha