IQNA

Kampeni ya Qur’ani Tukufu ya Fath: Qari wa Mauritania Awasilisha Qiraa

8:57 - August 10, 2025
Habari ID: 3481062
IQNA – Maqari kutoka mataifa mbalimbali wanaendelea kushiriki katika kampeni ya Qur’ani Tukufu ya Fath kwa kuwasilisha video za kisomo chao cha maneno ya Mwenyezi Mungu.

Ahmed Saud, qari kijana kutoka Mauritania, ni miongoni mwa washiriki hao, akisoma aya tukufu za Qur’ani zinazobeba maana ya ushindi na kufaulu, kwa sauti yenye khushuu na ufasaha wa kiislamu.

Kampeni hii, iliyoanzishwa na Shirika la Kimataifa la Habari za Qurani (IQNA), inahamasisha Waislamu kushiriki kwa kusoma aya maalum za Qurani Tukufu – ikiwemo Surah Al-Fath (aya 1–4), Surah An-Nasr, na aya ya 139 ya Surah Al-Imran.

Waandalizi wanasema usomaji huu unalenga kuwa nguvu ya kiroho kwa wapiganaji walioko mstari wa mbele, na pia kukuza ujumbe wa Qurani wa subira, msaada wa Mwenyezi Mungu, na ushindi wa haki juu ya batili.

Tuma usomaji wako kwa WhatsApp kupitia nambari: +989127397608

 

captcha