IQNA

Wairani milioni tano wanasubiri zamu kwa ajili ya safari ya Umrah

16:48 - August 30, 2025
Habari ID: 3481156
IQNA – Zaidi ya Wairani milioni tano wanasubiri kwa hamu nafasi yao ya kwenda kufanya ibada ya Umrah, afisa mmoja amesema.

Akbar Rezaei, Naibu wa Shirika la Hija na Ziara, amesema kuwa zaidi ya watu milioni tano waliojisajili tangu mwaka 2011 na kabla yake bado hawajatekeleza safari ya Umrah. Ameeleza kuwa hakutakuwa na usajili mpya hadi wale wote waliokwisha jisajili wapate nafasi ya kwenda kutekeleza ibada hiyo tukufu.

Kwa mujibu wa afisa huyo, Wairani wapatao 208,000 walifanya Umrah mwaka uliopita. Amesema kuwa wale waliopata vocha (yaani waliokwisha jisajili kwa ajili ya Umrah) wanaweza kuomba nafasi kwa msimu wa sasa au misimu ijayo, kulingana na hali zao binafsi, bei mbalimbali, na muda wa kukaa katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.

Kundi la kwanza la waumini wa Iran waliokwenda Umrah baada ya Hija ya mwaka huu 2025 waliondoka wiki iliyopita kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran kuelekea Madina.

Umrah ni ibada ya Sunnah inayopendekezwa kwa Waislamu, lakini si ya lazima kama Hija. Tofauti na Hija ambayo ni faradhi kwa kila Muislamu mwenye uwezo wa kimwili na kifedha mara moja tu maishani, Umrah inaweza kufanywa wakati wowote wa mwaka.

3494417

Kishikizo: umrah iran
captcha