IQNA

Turathi za Qur’ani za marehemu Qari Farajullah Shazli zahifadhiwa katika Idhaa ya Qur’an ya Misri

15:43 - August 16, 2025
Habari ID: 3481091
IQNA – Mkusanyiko wa turathi za kitamaduni na kazi binafsi za Qur’an za Marehemu Sheikh Farajullah Shazli, mmoja wa maqari mashuhuri wa Misri, umewasilishwa kwa Idhaa ya Qur’an ya nchi hiyo.

Mkusanyiko huu ulipeanwa kwa Idhaa ya Qur’ani kwa lengo la kuuhifadhi kwenye jumba la kumbukumbu la wasomaji wa Qur’an wa Misri, ambalo linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Huu ni sehemu ya juhudi za Shirika la Taifa la Vyombo vya Habari la Misri katika kuhifadhi urithi wa kidini na mafanikio ya kihistoria ya wasomaji wakuu wa Qur’an wa nchi hiyo.

Sherehe ya kuwasilisha mkusanyiko huu kwa Idhaa ya Qur’an ya Misri ilihudhuriwa na Ismail Dwidar, mkuu wa idara ya vyombo vya habari na mahusiano ya umma katika idhaa hiyo.

Kama sehemu ya maandalizi ya ufunguzi wa jumba la kumbukumbu, Idhaa ya Qur’an ya Misri tayari ilipokea baadhi ya mali za Sheikh Shaaban al-Sayyad na Sheikh Muhammad Ahmed Shabib, wasomaji wengine mashuhuri wa Misri.

Akiwa amezaliwa mwaka 1948, Shazli alikamilisha hafla ya Hifdhi ya Qur’an akiwa na umri wa miaka minane. Aliungana na Kituo cha Qur’an cha Misri mwaka 1971 na kuhitimu mwaka 1979.

Sheikh Shazli aliendelea na masomo yake katika Kitivo cha Sayansi za Kiarabu na Kiislamu, Al-Azhar, ambapo alipata shahada ya uzamivu  mwaka 2004.

Alikuwa Imamu wa Msikiti wa Ahmadi mjini Tanta na pia alifanya kazi kama balozi wa Qur’an katika nchi nyingi duniani. Alikuwa mwalimu wa Qur’an, qari wa kimataifa, hakimu, na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar.

Alisafiri kwenda nchi nyingi, ikiwemo Iran, kusoma Qur’an na kuhudhuria kama jaji kwenye mashindano ya kimataifa ya Qur’an ya Iran.

Sheikh Shazli, ambaye alikuwa naibu mkuu wa Shirikisho la Wasomaji wa Qur’an wa Misri, alifariki akiwa na umri wa miaka 69 katika kijiji cha Armania, Wilaya ya Beheira, kaskazini mwa Misri, mnamo Juni 5, 2017.

/3494271

captcha