IQNA

Ujumbe wa Iran watembelea Malaysia kuimarisha uhusiano wa kidini, kielimu na kitamaduni

17:11 - August 30, 2025
Habari ID: 3481159
IQNA-Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Iran, wakiongozwa na Ayatullah Alireza Arafi na Ayatullah Ahmad Mobaleghi, umefanya ziara ya siku tatu nchini Malaysia kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya muda mrefu ya kielimu na kidini kati ya mataifa hayo mawili.

Ziara hiyo ilihusisha ushiriki katika mikutano ya kielimu, kitamaduni na ya kidini, huku ikisisitiza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuleta umoja wa Kiislamu na kuunga mkono wanyonge, hasa watu wa Gaza.

Ayatullah Arafi alizungumza na wanazuoni wa Kimalay na Wairani wanaoishi Malaysia kuhusu mitazamo mitatu ya Uislamu wa kisasa: Uislamu wa kurudi nyuma, Uislamu wa kiliberali, na Uislamu wa kweli unaotegemea Qur’an, Sunnah, akili na ijtihad. Alisisitiza umuhimu wa utambulisho wa Kiislamu wa pamoja, bila kujali taifa la mtu.

Ujumbe huo ulihudhuria Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Viongozi wa Kidini ulioandaliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, ambapo viongozi zaidi ya 1,000 kutoka nchi 54 walishiriki. Mkutano huo ulijadili masuala ya umoja, msaada kwa Waislamu wa Palestina, na jukumu la dini katika kuondoa migogoro.

Viongozi hao pia walikutana na Waziri wa Masuala ya Kidini wa Malaysia na Waziri Mkuu Anwar Ibrahim, wakijadili ushirikiano wa kielimu na wa Qur’ani. Walihudhuria swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Velayat na kukutana na Mufti wa Kuala Lumpur. Mkutano na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Dunia pia ulifanyika, pamoja na ziara katika taasisi za kielimu na mikutano na Wairani waishio Malaysia.

3494421

Habari zinazohusiana
captcha