IQNA

Wayemen waandamana kulaani uchomaji wa nakala ya Qur’ani Marekani na ukatili wa Israeli Gaza

17:25 - August 30, 2025
Habari ID: 3481160
IQNA – Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Yemen walifanya maandamano makubwa siku ya Ijumaa kulaani uhalifu wa Israeli dhidi ya Wapalestina na kitendo cha hivi karibuni cha kuchomwa motot nakala ya Qur’an Tukufu nchini Marekani.

Maandamano hayo makubwa yalifanyika chini ya kauli mbiu: “Pamoja na Gaza: Jihadi na Msimamo Thabiti… Hasira kwa Damu Iliyomwagika na Heshima Kwa Waliodhalilishwa.” Yalifanyika katika mji mkuu wa Sana’a na mikoa mbalimbali ya Yemen, yakilaani uhalifu unaoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza, na kusimama kidete kutetea Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungum, yaani Qur'ani Tukufu, huku wakilaani  mwanasiasa mwenye mwelekeo wa Kizayuni nchini Marekani ambaye alitetekteza moto nakala ya Qur'ani Tukufu.

Umati wa Wayemen waliobeba nakala za Qur’an walithibitisha utayari wao wa kuilinda Qur’an Tukufu na Msikiti wa Al-Aqsa. Wamesema mashambulizi ya Kizayuni dhidi ya maeneo haya matakatifu ni ushahidi wa chuki ya kina na uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Washiriki walilaani kimya cha tawala za nchi za Kiarabu na Kiislamu mbele ya dhulma hizi na matusi dhidi ya alama na heshima za Uislamu, wakisisitiza kuwa asiyeguswa na dhulma dhidi ya Qur’ani na maeneo matakatifu hawezi kuwa na msimamo wa kweli dhidi ya mpango wa upanuzi wa Kizayuni, hata kama utamfikia mlangoni mwake.

Kwa kujitokeza kwa wingi mtaani—siku moja tu baada ya shambulio la anga la Kizayuni kulenga maeneo ya raia Sana’a—Wayemen walituma ujumbe wa ujasiri kwa adui wa Muisraeli na washirika wake, wakithibitisha kuwa vitisho na njama, hata ziwe kali kiasi gani, haviwezi kuyumbisha msimamo wa Yemen wa kuunga mkono watu wa Palestina na mapambano yao ya kishujaa.

“Watu wa Imani na Hekima” walikumbusha uhusiano wao wa kina na usiotenganika na Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Kitabu Chake, na azma yao ya kuendelea na njia ya jihadi na mapambano kutetea maslahi na heshima za Ummah, wakikabiliana na njama zote za maadui wake.

Waandamanaji pia walilaani kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kusitisha janga la kibinadamu linalosababishwa na utawala wa Israel huko Gaza, likielezewa kuwa baya Zaidi, kutokana na hali mbaya ya kibinadamu na kiafya inayotokana na njaa ya makusudi, kuzuia misaada na dawa, sambamba na kampeni ya mabomu inayoharibu Ukanda mzima wa Gaza.

Umati huo ulipandisha bendera za Yemen na Palestina, pamoja na mabango ya kuukaribisha mwezi wa kuzaliwa kwa Mtume wa Rehema na Ubinadamu, Muhammad Al Mustafa (SAW). Walionesha furaha na uaminifu wao kama kizazi cha Ansar, wakithibitisha mapenzi yao kwa Mtume Mtukufu (SAW) na ufuasi wao kwa njia yake.

3494419

Habari zinazohusiana
captcha