iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Uingereza imetakiwa kuwapa Waislamu ulinzi kufuatia hujuma za Ijumaa iliyopita dhidi ya misikiti miwili nchini New Zealand.
Habari ID: 3471882    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/20

TEHRAN (IQNA)-Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina Michael Lynk amesema upokonyaji wa maliasili za Wapalestina unaofanywa na utawala haramu wa Israel katika maeneo ya Palestina ni uporaji wa wazi.
Habari ID: 3471881    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/19

TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Malaysia Mahathir Mohammad amesema baadhi ya Waislamu hawana ufahamu sahihi wa Qur'ani na hivyo wanajihusisha na vitendo vilivyo kinyume cha mafundisho ya Uislamu.
Habari ID: 3471880    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/18

TEHRAN (IQNA) – Pale waumini walipokuwa wakimiminiwa risasi na gaidi wakati wa Sala ya Ijumaa msikitini, dereva wa texi, Abdul Kadir Ababora, alijificha chini ya rafu ambayo hutumika kuweka nakala za Qur'ani Tukufu huku akiomba Duaa kuwa apate fursa ya kubakia na mke na watoto wake.
Habari ID: 3471879    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/17

TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hujuma za kigaidi zilizolenga misikiti miwili jana mjini Christchurch New Zealand na kupelekea Waislamu wasiopungua 49 kuuawa shahidi wakiwa katika Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3471878    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/16

TEHRAN (IQNA)- Waislamu wasiopungua 49, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wameuawa na wengine wasiopungua 48 wamejeruhiwa katika hujuma za kigaidi zilizofanywa dhidi ya misikiti miwili katika mji wa Christchurch nchini New Zealand wakati waumini wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya Sala ya Ijumaa hii leo.
Habari ID: 3471877    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/15

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asema:
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kwamba adui mkuu wa taifa la Iran ni Marekani na kwamba kamwe taifa hili halitafanya kosa katika kumfahamu adui huyo.
Habari ID: 3471876    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/15

TEHRAN (IQNA)-Nchi 82 zinatazamiwa kuwa na wawakilishi katika Mashidani ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran mwaka huu.
Habari ID: 3471875    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/14

TEHRAN (IQNA)- Watoto wa shule moja ya chekechea ya Wakristo mjini Dusseldorf nchini Ujerumani wataanza kufunzwa Uislamu.
Habari ID: 3471872    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/12

TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Elimu wa Iran Sayyid Mohammad Bathayi amesema takribani wanafunzi zaidi ya milioni mbili nchini Iran wanashiriki darsa za kuhifadhi Qur'ani.
Habari ID: 3471871    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/11

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Marekani wanabaguliwa zaidi ya wafuasi wa dini zingine zote nchini humo.
Habari ID: 3471870    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/10

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu kuwepo uthabiti na amani nchini Myanmar. Aidha amesisitiza kuwa wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya warejeshwe haraka na kwa usalama katika makazi yao nchini Myanmar.
Habari ID: 3471869    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/09

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, Marekani ilikuwa na njama kubwa tofauti kwa ajili ya kusambaratisha harakati hiyo mwaka 2006, lakini uimara wake umeweza kusambaratisha njama zote hizo.
Habari ID: 3471868    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/09

TEHRAN (IQNA)-Wananchi wa matabaka mbali mbali huko Algeria wameendeleza maandamani Ijumaa wakimtaka Rais Abdelaziz Bouteflika aondoke madarakani na asiwanie tena urais mwezi ujao wa Aprili.
Habari ID: 3471867    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/08

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Sudan imetangaza azma yake ya kuunga mkono madrassah za Qur'ani nchini humo ili kuhakikisha zinafanikiwa katika kustawisha elimu ya Qur'ani.
Habari ID: 3471864    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/06

TEHRAN (IQNA)- Sheikh Mkuu wa Al-Azhar wa Al Azhar amekosolewa na wanazuoni wenzake wa Kiislamu nchini Misri kwa kudai kuwa "ndoa ya wake wengi ni dhulma kwa wanawake na watoto".
Habari ID: 3471863    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/05

Mufti Mkuu wa Russia
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wanatarajiwa kuongezeka na kufika asilimia 30 ya watu wote wa Russia ifikapo mwaka 2034 na hivyo kuna haja ya kujenga misikiti zaidi nchini humo.
Habari ID: 3471862    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/05

TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika mji wa Memphis jimboni Tenessee wameanza chehreza za muda wa mwezi moja kwa lengo la kuutmabulisha Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu eneo hilo.
Habari ID: 3471861    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/04

TEHRAN (IQNA) –Wataalamu 22 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 13 za kigeni wameteuliwa kuwa majaji katika Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3471859    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/03

TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Misri inatekeleza mpango wa majaribio wa adhana ya pamoja katika misikiti 113 nchini Cairo ili kuzuia sauti mbali mbali katika vipaza sauti vya misikiti wakati wa adhana.
Habari ID: 3471858    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/02