iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 9 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Kuwait, maarufu kama Zawadi ya Kuwait, yalianza Jumanne katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Habari ID: 3471462    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/12

TEHRAN (IQNA)- Wanaharakati wa Akademia katika Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Jumanne wameandamana wakitaka serikali imiachilie kiongozi wao aliye kizuzizini Sheikh Ibrahim Zakzaky huku aachiliwe huru mara moja.
Habari ID: 3471461    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/11

TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa kwanza kujengwa katika eneo la Outer Hebrides huko Scotland nchini Uingereza utafunguliwa katika kipindi cha miezi michahce ijayo hata baada ya Kanisa la Presbyterian kupinga vikali ujenzi huo.
Habari ID: 3471460    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/10

TEHRAN (IQNA)-Chama cha Barisan Nasional nchini Malaysia kimetangaza mpango wa kujenga Chuo Kikuu cha Qur'ani nchini humo ambapo watakaohitimu hapo watakuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na pia watakuwa wamepata utaalamu katika taaluma nyinginezo.
Habari ID: 3471459    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/09

Taasisi ya Darul Iftaa ya Misri
TEHRAN (IQNA)- Taasisi ya Darul Iftaa ya Misri, ambayo hutoa muongozo wa Kiislamu nchini humo, imetangaza kuwa mchezo maarufu wa video wa ‘Blue Whale’ ni haramu katika Uislamu baada ya kubainika kuwa watu kadhaa walioucheza wameishia kujitoa uhai.
Habari ID: 3471458    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/08

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Jimbo la Texas nchini Marekani imetangaza zawadi ya $5000 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa mtu ambaye alimdunga kisu mwanamke Mwislamu katika mji wa Houston.
Habari ID: 3471457    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/07

TEHRAN (IQNA)-Nchi 23 zimetangaza azma ya kushiriki katika Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baadaye mwezi huu.
Habari ID: 3471455    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/06

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo msimamo wa daima wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuiunga mkono kikamilifu Palestina na wapiga jihadi wake na kusema kuwa, tiba ya kadhia ya Palestina ni kuimarisha mrengo wa mapambano na muqawama katika Ulimwengu wa Kiislamu na kuzidisha mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na waungaji mkono wake.
Habari ID: 3471454    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/05

TEHRAN (IQNA)-Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri imetangaza kukamilika tarjuma mpya ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili.
Habari ID: 3471453    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/04

TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Ardhi yalifanyika leo kwa siku ya nne mfululizo huko katika Ukanda wa Gaza na kushambuliwa tena na askari wa utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3471451    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/02

TEHRAN (IQNA)-Mtoto mwenye ulemavu wa machi Misri amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamlifu kwa lugha asi ya Kiarabuna pia kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa.
Habari ID: 3471450    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/01

TEHRAN (IQNA)-Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Misri wametangazwa ambapo ambapo Ustadh Haitham Sagar kutoka Kenya ameibuka wa pili katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kwa wale ambao Kiarabu si lugha yao ya asili.
Habari ID: 3471449    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/31

TEHRAN (IQNA)-Uturuki imewatunuku Waislamu wa kusini mwa Uhispania nakala 3,000 za Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3471448    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/30

TEHRAN (IQNA)- Mhadhiri wa Uislamu kutoka India amesema Qur'ani Tukufu ni muongozo kamili kwa wanadamu wa zama zote.
Habari ID: 3471447    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/29

TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 9 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Kuwait yanatazamiwa kuanza katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi mnamo Aprili 10.
Habari ID: 3471446    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/28

TEHRAN (IQNA)- Nusu Fainali ya Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu imemalizika.
Habari ID: 3471445    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/27

TEHRAN (IQNA) – Misikiti mitatu ilihujumiwa katika maeneo tafauti ya Ujerumani siku ya Jumapili katika kile kinachoonekana na kuongezeka hisia za kuuchukuia Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3471444    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/26

TEHRAN (IQNA)-Baraza la Kimataifa la Wahudumu wa Qur'ani Tukufu limeasisiwa nchini Misri katika kikao kilichohudhuriwa na wataalamu na wanaharakati wa Qur'ani.
Habari ID: 3471443    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/25

TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza leo asubuhi mjini Cairo ambapo yanahudhuriwa na wawakilishi wa nchi 50.
Habari ID: 3471442    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/24

TEHRAN (IQNA)- Msikiti katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm, umehujumiwa na kuandikwa maandishi na nembo za kibaguzi siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3471441    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/03/23