chuki dhidi ya uislamu - Ukurasa 14

IQNA

IQNA: Serikali ya Afrika Kusini imesema chuki dhidi ya Uislamu ndio chanzo cha hujumza mbili dhidi ya misikiti mjini Cape Town.
Habari ID: 3470793    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/01/14

IQNA-Waislamu wawili wametimuliwa kutoka ndege ya shirika moja la Marekani mjini London baada ya wasafiri kadhaa Waingiereza kulalamika kuwa walimsikia mmoja wao akizungumza kwa lugha ya Kiarabu kwa simu.
Habari ID: 3470753    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/12/22

IQNA-Mbunge mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi amepatikana na hatia ya kuwatusi watu wenye asili ya Morocco na kuwabagua.
Habari ID: 3470728    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/12/09

IQNA-Viongozi wapatao 300 wa jamii ya Waislamu nchini Marekani wamemwandikia barua ya wazi Rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump likiwa ni jibu kwa matamshi ya chuki aliyotoa dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3470721    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/12/06

IQNA-Zaidi ya zaidi ya vituo vya Kiislamu na misikiti 100 imehujumiwa nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Habari ID: 3470690    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/11/22

IQNA-Kumeshuhudiwa wimbi la hujuma dhidi ya Waislamu kote Marekani baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais siku ya Jumanne.
Habari ID: 3470666    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/11/11

Mwanamke Mwislamu amehujumiwa na kuvuliwa Hijabu katika hujuma ya kibaguzi iliyojiri mjini London.
Habari ID: 3470607    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/10/10

Seneta Pauline Hanson wa Australia amekosolewa kwa matamshi yake yaliyojaa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Habari ID: 3470568    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/17

Wakaazii wa mji wa Tshwane nchini Afrika Kusini wamebainisha hasira zao baada ya kupatikana maandishi ukutani yenye kuwavunjia heshima Waislamu.
Habari ID: 3470566    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/16

Katika kitendo kingine cha chuki dhidi ya Waislamu, mwanamke aliyekuwa amevaa Hijabu ameshambuliwa na kuchomwa moto mjini New York, Marekani.
Habari ID: 3470562    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/14

Kituo cha Kiislamu katika jimbo la Florida Marekani kimeteketezwa moto na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3470561    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/09/13

Imam wa msikiti mmoja katika jimbo la New York nchini Marekani ameuawa kwa kufyatuliwa risasi katika hujuma ya kigaidi.
Habari ID: 3470522    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/14

Wanafunzi Wakristo nchini Zimbabwe wameshiriki katika warsha ya siku moja kuhusu Uislamu.
Habari ID: 3470510    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/09

Wanandoa Waislamu wamelituhumu Shirika la Ndege la Marekani la Delta Airlines kwa kuwa na chuki dhidi ya Uislamu baada ya kuwazuia kusafiri na ndege ya shirika hilo mjini Paris.
Habari ID: 3470497    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/08/06

Mamia ya watu, wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu wameandamana Marekani kupinga chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu au Islamophobia..
Habari ID: 3470470    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/07/24

Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa katika ufyatuaji wa risasi uliotokea katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Habari ID: 3470382    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/13

Ofisa mwenye cheo cha meja katika jeshi la Marekani amekamatwa baada kujaribu kuwaua msikitini na kuwazika hapo katika jimbo la Carolina Kaskazini.
Habari ID: 3470377    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/11

Waislamu nchini Marekani katika jimbo la New Mexico wametangaza kuimarisha harakati za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).
Habari ID: 3470364    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/07

Chuki dhidi ya Uislamu
Kundi la wanaume jimboni Texas nchini Marekani wanapata mafunzo maalumu kwa ajili ya kuwaua Waislamu huku wakitumbukiza risasi zao katika damu au mafuta ya nguruwe katika mazoezi hayo.
Habari ID: 3470345    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/29

Waislamu nchini Marekani wanakabiliana na wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia hata baada ya kuwa wamelaani vikali hujuma ya kigaidi mjini Brussels, Ubelgiji Jumanne hii.
Habari ID: 3470215    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/26