IQNA

Mwenye Chuki kwa Uislamu Uholanzi apatikana na hatia lakini hakuadhibiwa

18:31 - December 09, 2016
Habari ID: 3470728
IQNA-Mbunge mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi amepatikana na hatia ya kuwatusi watu wenye asili ya Morocco na kuwabagua.

Kwa mujibu wa mashtaka dhidi ya Wilders, katika mkutano wa kampeni mwaka 2014 aliongoza wafuasi wake waliokuwa wakitoa nara za kutaka Wamorocco wanaoishi nchini Uholanzi waondoke. Wilders ambaye hakuhudhuria kikao hicho cha mahakama amesema atakata rufaa kuhusu hukumu hiyo.

Majaji hawakumuadhibu Geert Wilders kwa madai kuwa kupatikana na hatia ni adhabu tosha.

Mwendesha mashtaka wa Uholanzi ambaye alitaka Wilders atozwe faini ya Euro 5000 naye pia amedai kupatikana na hatia ni muhimu hata kuliko adhabu na hivyo ameafiki uamuzi wa majaji wa kutotoa adhabu ya kifungo cha jela wala faini kwa mwanasiasa huyo mwenye misimamo ya chuki dhidi ya Waislamu.

Wilders ambaye hakuhudhuria kikao hicho cha mahakama amesema atakata rufaa kuhusu hukumu hiyo.

Baadhi ya weledi wanasema hukumu hiyo itampa msukumo Wilders ambaye anataka chama chake kinachojiita Freedom Party kipate wingi wa krua katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Chama hicho chenye misimamo ya kufurutu ada ya mrengo wa kulia kinaendelea kupata umashuhuri Uholanzi kutokana na kukita mizizii hisia za chuki dhidi ya wageni na Waislamu nchini humo na kote Ulaya.

Akizungumza mwezi Agosti mwaka huu, Wilders alisema kuwa, endapo chama chake kitashinda katika uchaguzi ujao, kitachukua maamuzi makali dhidi ya Waislamu.

Wilders alisisitiza kupitia taarifa ya kichochezi kuwa, kama atakuwa waziri mkuu wa Uholanzi, atapiga marufuku Qur'an tukufu na kufunga misikiti yote nchini humo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Wilders kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu. Kile kilichopelekea jina la Wilders kupata umashuhuri katika miaka ya hivi karibuni ni hatua yake ya kutengeneza filamu ya kuivunjia heshima Qur'an Tukufu ambacho ni kitabu cha mbinguni cha Waislamu, filamu iliyoitwa jina la 'Fitina.'

Utengenezwaji wa filamu hiyo uliibua malalamiko ya Waislamu duniani kote na hata kufunguliwa mashtaka dhidi ya mwanasiasa huyo katika mahkama za Uholanzi.

Kufuatia ushindi wa Donald Trump mwenye chuki dhidi ya Uislamu katika uchaguzi wa rais Marekani, wanasiasa wenye misimamo mikali ya mrengu wa kulia kote Ulaya nao pia wamepata matumaini ya kunyakua madaraka.

Uholanzi inatarajia kufanya uchaguzi wa bunge hapo mwezi Machi mwakani. Kwa kuzingatia wimbi la uhajiri kuelekea barani Ulaya ambalo limeibua tatizo kubwa katika mwenendo wa maisha ya kindugu barani humo, suala hilo limegeuzwa kuwa moja ya maudhui kuu zinazojadiliwa katika kampeni za uchaguzi.

3552335


captcha